Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mijadala kuhusu Tanzania kuruhusu uraia pacha. Wapo wanaopendekeza Tanzania kama nchi ikubali uwepo wa uraia pacha ili kuzipata faida zitokanazo na uraia wa aina hiyo. Wapo wenye mtazamo kuwa muda wa Tanzania kuwa na uraia pacha bado haujafika. Hivyo basi, wanauunga mkono msimamo wa Serikali wa kutokubali na kuanzisha uraia pacha hapa nchini.
Uraia ni jambo la kisheria. Endapo Serikali itaridhia kuanzishwa kwa uraia pacha, lazima sheria inayosimamia masuala ya uraia ifanyiwe marekebisho kukidhi matakwa ya mabadiliko hayo. Ilivyo sasa, uraia unaokubalika hapa nchini ni uraia wa nchi moja: kama ni raia wa Tanzania au la. Raia wa Tanzania, ilivyo sasa, haruhusiwi kuwa raia wa nchi nyingine yeyote duniani. Ikitokea hivyo, raia husika itampasa kupoteza uraia mmojawapo: ima wa Tanzania au wa hiyo nchi nyingine.
Kwa kuwa mimi si mbobezi wa masuala ya kimataifa na kiuraia na naamini JF ni nyumba ya wabobezi wa mambo hayo na mengine, naomba kuwasilisha hoja na wito kwa waungwana kuziainisha faida na hasara za kuwa na uraia pacha hapa nchini kwetu Tanzania. Kujua faida na hasara kutachochea au kupooza wito wa wananchi wa kutaka uwepo wa uraia pacha kwa watanzania.
Karibuni waungwana wa JF...