Mangisandy
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 2,652
- 2,273
Au visevesa! Kwanini usiamini kwamba watutumia hizo fursa kutunufaisha Sisi?Hatutaki uraia chotara. Kama ilivyo kwa mtu chotara anajipendekeza kwa mbari nyeupe na kujiweka mbali na watu weusi. Tabia yao wengine ni wabaguzi kuliko mtu mzungu au mwarabu. Vivyo hivyo uchotara wa uraia mtu utamkuta kujifanya mzalendo uzunguni au uarabuni. Wanaweza kutumia haki za uraia afrika kwa faida ya huo uraia wake wa kizungu au asia kwa kuzifaidisha nchi zingine na kuwafukarisha wenyeji wa nchi yake asili.
Kwanza kabisa nimemkosoa Wakili msomi, tayari tuna dual citizenship Tanzania! Hujaona kama hiyo ni point?!Unaona sasa, yaani pro dual citizenship hamnaga hoja.
Sasa hapa umeongea nini?
Ujamaa ni msingi wa haya maamuzi ya kukataa uraia pacha. Bado kuna zile mentalities za Nyerere kwamba adui mbaya hayupo kati yetu bali ni yule anayetokea nje.Kwa nchi, kiuchumi, uraia pacha karibu mara zote ni mzuri zaidi ya uraia wa nchi moja tu.
Kwa mtu, inategemea na kipaumbele cha mtu.
Kwa mfano, Mtanzania mwenye uraia wa Marekani pia, ambaye ana malengo ya kuwekeza Tanzania, anaweza kuona uraia pacha ni kitu cha muhimu kwa sababu ya malengo yake ya uwekezaji.
Kiujumla, uraia pacha una faida nyingi kiuchumi kwa sababu utawapa Watanzania wenye uraia wa nchi nyingine nafasi kubwa ya kuwekeza nchini.
Hili jambo lilijadiliwa sana. Serikali ya Mkapa ikalikataa. Kwa sababu ambazo zilielezwa kuwa za usalama, lakini zilikuwa za kisiasa zaidi. Watu wenye uraia wa nchi nyingine walionekana kuwa na upeo mkubwa wa mambo kutokana na kuishi nje, wakaonekana tishio kwa utawala wa CCM.
Mkapa alisema ameridhia kuona Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine wanapewa "permanent residence" status Tanzania, waweze kuingia na kutoka bila visa, na wapewe upendeleo wa kuwekeza sawa na raia, lakini wadhibitiwe wasijiingize kwenye siasa.
Kuna Mzee mmoja niliongea naye akasema kuna Watanzania wengi wana hulka ya wivu tu, akasema hata enzi zao walivyokuwa wanafanya kazi Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuna Wakenya na Waganda wengi walikuwa wanatafutiana fursa za kwenda nje, lakini Watanzania walikuwa wanazibiana. Mtu akitaka kwenda nje kujiendeleza alikuwa anaonekana kama msaliti.
Ndiyo mpaka leo kuna huo ujinga, mtu akichukua uraia wa nchi nyingine, hata kwa kutafuta maisha tu, anaonekana si mzalendo, tishio, beberu na ujinga mwingine mwingi kama huo.
Wakati kiuhalisia mtu anayechukua uraia wa nchi nyingine ndiye anayeweza kuisaidia nchi zaidi.
Kuna wakati nilikuwa nafanya kazi Wall St. recruiters wakaiona resume (C.V) yangu, wakaipenda. Wakasema wana kazi Federal Reserve (Benki Kuu ya Marekani) wanataka kuniunganishia.
Nikawaambia sawa, lakini kwanza kabisa nikasema nataka kuwaambia kuwa mimi si raia wa Marekani (muda huo sijachukua uraia bado, nasubiria habari za uraia pacha Tanzania).
Recruiters wakaniambia, hilo si tatizo, tuachie sisi.
Nikawauliza, kweli? Mbona mimi ninavyojua position nyeti kama hii Benki Kuu ya Marekani itataka mtu aliye raia tu?
Wakasema tuachie sisi.
Nikasema sawa.
Wakaenda kuulizia vizuri zaidi, wakarudi.
Wakasema, ulivyosema ni kweli.
Ile kazi una kila sifa, ungefaa sana. Tatizo wanataka raia wa Marekani.
Nikasema mimi nilijua hilo. Nikawashukuru.
Nikaona kusubiri uraia pacha ni ujinga, after all, mimi niliamua kuhama kimoja kuja Marekani. Sijaja Marekani kwa lengo la kuishi na kurudi Tanzania.
Baada ya kusubiri uraia pacha kwa miaka 15, nikaamua kuchukua uraia wa Marekani.
Ukiangalia hapo, utaona kwamba, Tanzania imejinyima nafasi ya kuwa na raia wake anayefanya kazi Benki Kuu ya Marekani, anayeweza kuona mambo yanavyoenda huko Benki Kuu ya Marekani na kuisaidia Tanzania kwa ujuzi wake anaoupata huko.
Kukosa kuelewa.Anayeweza kuwa na uraia pacha ni yule aliyekuwa mtanzania kutoka awali.Hivyo Mkenya hana nafasi ya kuwa na uraia pacha.ukiruhusu uraia pacha wakenya watakuja kutuchukulia ardhi yetu yote, Watanzania Tutakuwa wapangaji.
Wrong.Somalia mtu mwenye uraia pacha anaweza kuwa Rais ikiwa tu asili yake ya mwanzo ni mzaliwa wa Somalia yaani hajazaliwa nje ya Somalia.Hasara: Mtu mwenye Raia pacha hawezi kuwa Rais wa Nchi yoyote, hivyo unaweza kosa kiongozi mzuri kutokana na jambo hilo.
Hiyo safiWrong.Somalia mtu mwenye uraia pacha anaweza kuwa Rais ikiwa tu asili yake ya mwanzo ni mzaliwa wa Somalia yaani hajazaliwa nje ya Somalia.
Sisi tunapata "the worst of both worlds".Ujamaa ni msingi wa haya maamuzi ya kukataa uraia pacha. Bado kuna zile mentalities za Nyerere kwamba adui mbaya hayupo kati yetu bali ni yule anayetokea nje.
Wizi mkubwa mkubwa kama ule wa EPA, ESCROW wahusika ni watanzania wenye kuishi humu humu nchini waliolelewa wakiambiwa mzalendo ni wa ndani na wa nje ni adui.
Tutakuja kubadilika kwani kuna ongezeko kubwa la watanzania wa diaspora na ndipo tutakapogundua ukubwa wa fursa tulizozipoteza kwa miaka mingi.
Hivi huo uraia mutaugawa kama njugu? Jifunzeni kwa wakoloni wetu- wao wanaruhusu hata uwe na passports 195 ili mradi tu ufuate sheria yao ya kuishi kwao... hakuna bugudha... kama Tanzania tumeshindwa kutengeneza sheria yetu inayo ruhusu uraia Pacha basi tujifunze kwa majirani au wakoloni wetu wa zamani... duniani humu hakuna cha uzalendo wala nini, ni maslahi tu ndio yanazungunza- kuanzia ngazi ya familia hadi taifa ni maslahi tu... ya nini kuoneana wivu na kuyafanya maisha magumu? Tusaidianeni bila vikwazo ndio tutasonga mbele kama nchiukiruhusu uraia pacha wakenya watakuja kutuchukulia ardhi yetu yote, Watanzania Tutakuwa wapangaji.
Huo ushahidi uko wapi? Na kwa nini iwe rahisi kihivyo? Au watunga sheria watakuwa fofofo?ukiruhusu uraia pacha wakenya watakuja kutuchukulia ardhi yetu yote, Watanzania Tutakuwa wapangaji.
Itategemea na maslahi- huwa wanaangalia ukisafiri kwa passport ipi...Nilivyokuelewa, uraia wa nchi moja ni bora zaidi ya uraia pacha. Ni sawa?
Leo kwa mada hii, tupo pamoja! Nakupa like!Kijana wangu nashukuru kwa kuleta mada hii namimi napenda kuchangia ili kutoa elimu;
Faida za uraia Pacha; humuwezesha mtu kupata huduma za kijamii nchi yoyote ambayo ana uraia.Kama uraia wa Tanzania na Marekani,utanufaika na kupata elimu,huduma za afya bila kubaguliwa. Kwa Mtanzania mwenye uraia pacha hapa hunufaika na huduma bora toka nchi zilizoendelea na kuna fursa ya nchi kama Tanzania kunufaika na utaalamu na ujuzi wa raia hawa waliopata ujuzi nje ya nchi na pia kwa upande wa gharama za matibabu hili litaweza kupunguza gharama kwa Tanzania.
Pili,mtu mwenye uraia pacha anaweza kupiga kura au kuligiwa kura kupata uongozi nchi yoyote. Hapa kuna fursa kwa nchi kwamba kama mtu huyu ana utaalam na hana nia mbaya atakuwa msaada lakini kama mtu huyu atakuwa na nia mbaya au ni pandikizi kuna hatari kubwa ya sana kiusalama.Ni ngumu kutambua je huyu mtu ni mtiifu kwa taifa gani?
Tatu,mtu mwenye uraia pacha huweza kumiliki mali katika nchi yoyote atakayo.Ni fursa kwamba mali hususani nyumba kupata soko la uhakika ila kuna hatari ya kwamba watu hususani pale anapokuwa na maslahi ya kihasusi kununua mali na kisha kutozitumia,hii huathiri uchumi au kuitumia kwa maslahi ya ujasusi ya nchi nyingine.
Nne, mtu mwenye uraia pacha analipa kodi kwa zote ambazo ana uraia.Kwa nchi kama Tanzania hii ni fursa ya kukusanya kodi kutoka kwa madiaspora wote waliopo ulimwenguni.
Pole kwa kuikosa hiyo kazi ya maana huko US.Sisi tunapata "the worst of both worlds".
Yani kwenye kufuata Ujamaa hatupo kamili, tunapata mabaya ya kufuata Ujamaa, bila kupata mazuri ya kufuata Ujamaa.
Ndipo hapo unakuta mambo ya low investment, kuogopa "maadui wa nje", bila subsidized healthcare, education etc
Kwenye Ubepari nako hatupo kamili, tunapata mabaya ya Ubepari bila kupata mazuri ya ubepari.
Ndipo hapo unakuta watu wameuziana nyumba za umma, wameuziana viwanda, wamepiga hela EPA bila kuzuiwa na mazuri ya ubepari kama free press, labor unions, strong opposition, open market etc.
Tunapigwa kutoka pande zote.
Kama nchi, tutapata hasara za kutokuwa na uraia pacha kwa kukosa connections za maana na investment, bila kupata faida za kuwa na uraia mmoja tu ambazo ni za mazingaombwe zaidi.
Wewe nchi mpaka utawala wa Kikwete Ikulu ilikuwa inatumia email ya Yahoo, hapo unahitaji raia wa kigeni aingie nchini kuku compromise?
Kila siku tunasikia watu wanafanya mambo mitandaoni, bado watu wanashikilia uraia kuwa ndiyo kitu kitakachowahakikishia usalama?
Kiranga amemwaga material za maana sana, Philippe! Soma tena umpe like yake!Pole kwa kuikosa hiyo kazi ya maana huko US.
Kiukweli pro dual citizenship wa Tanzania hawana hoja za maana ndio maana hawaeleweki.
Na wengi wanaotoa hoja, wanagusia sana maslahi binafsi jambo ambalo ni gumu kushawishi watu wawaelewe. Ni sawa na mtu aende kutafuta kazi halafu sababu anasema anataka kusaidia familia yake.
Ifahamike nchi yetu bado changa na wabongo bado mbumbumbu na uwezo mdogo.
Silaha yetu kubwa kwasasa bado ni ARDHI kitu ambacho nchi nyingi zinazotuzunguka hazina.
Siku ukienda hapo Kenya ndio utajua thamani ya ardhi.
Tanzania ina takribani watu 60M hivi sasa na wanaongezeka kila siku. Unfortunately ardhi haiongezeki.
Na ukisema uruhusu uraia pacha with some limitations hasa kwenye ardhi au utawala hawa pro dual citizenship wanaweza wasikuelewe kwasababu wanachokitaka utakuwa umeziba.
Ni sawa na EAC kutaka eti mtu yeyote ndani ya jumuiya ya Africa Mashariki aruhusiwe kwenda kuishi popote ndani ya jumuiya. Wanaotunga sera hiyo wao ardhi hawana.
Muhimu ni kwanza sera zibadilike hasa za ardhi, either kila mtu apewe chake then ndio tuwe free kugawa uraia.
Au vile vile tunaweza pia kutoa Uraia pacha kwa watu wachache wenye uwezo wa kuwekeza kiwango fulani cha pesa kama $500,000+ na siyo kwa kila Tom and Jerry.
What a load of trollop. Raia ni raia, iweje tena kuwe na mipaka? Inapofika vita vya Nduli Iddi Amin, mathalani, tukitakuwa kuchangia damu, si anaweza kusema kuwa mue sina ardhi? Kama huko atokako ana ardhi, atawapenda zaidi? Sikubta Olympic atachezea njinipu? Kwa nini inapojiri asiibe ndege zetu na makanikia yetu kama kina tundulissu na fatmakarume kuwatetea mabeberu KKY (kama kwaida yao)? Tumefunga Serengeti kupitia Bologonja au Mlina Kilimsnharo kutojea Tsavo, kama yeye ni raia kwa nini asipite na watalii wake? Imagine if a man and his wife have dual marriages, I mean, married in each dual country, itakuwaje?Siyo kweli. Kila nchi inaporuhusu uraia pacha huweka sheria kulingana na maslahi yake. Kwa mfano Tanzania ikiruhusu uraia pacha inaweza kuweka sheria kuwa mtu ambaye siyo mzaliwa wa Tanzania na hata kama atapata uraia wa kuomba anaweza kufanya mambo A,B,C, na hawezi kufanya mambo C,D,E,. Hata USA wanaruhusu uraia pacha lakini kuna mambo mengine kama swewe siyo raia wa kuzaliwa wa USA huwezi kuyafanya. Ni kiasi cha kuweka mipaka tu.
Mimi nilikuwa na kazi yangu nzuri tu nafanya, hao recruiters wakawa wananitaka, kwa hiyo niliendelea tu na kazi yangu.Pole kwa kuikosa hiyo kazi ya maana huko US.
Kwanza, kwa taarifa yako Wakili msomi, Tanzania kisheria ina ruhusu kwa na uraia pacha, hata mtoto wangu ni raia wa Tanzania na nchi ya ng’ambo aliko zaliwa!
Kuanzaia kuzaliwa mpaka miaka 18, unaweza kuwa na uraia wa Tanzania na nchi nyingine ila, sifa hiyo itakoma, ukifikisha miaka 18!
Pili, nafikiri kuna faida kubwa zaidi kwa nchi yetu kuwa na uraia pacha kuliko hasara. Kwa mfano, mtoto wangu amezaliwa USA, kuna masilahi binafsi mengi kwake, kuwa Mmarekani, kuliko kuchagua Utanzania!
Lakini kiuhalisia, amezaliwa Marekani ni raia, ana wazazi Watanzania, ni Mtanzania! Sheria inatakiwa ivuke mipaka imfuate mtoto wangu, na siyo kumlimiti!
Aliyeelewa huu upuuzi anisaidie 🤣🤣🤣tukitakuwa kuchangia damu, si anaweza kusema kuwa mue sina ardhi? Kama huko atokako ana ardhi, atawapenda zaidi? Sikubta Olympic atachezea njinipu? Kwa nini inapojiri asiibe ndege zetu na makanikia yetu kama kina tundulissu na fatmakarume kuwatetea mabeberu KKY (kama kwaida yao)? Tumefunga Serengeti kupitia Bologonja au Mlina Kilimsnharo kutojea Tsavo, kama yeye ni raia kwa nini asipite na watalii wake? Imagine if a man and his wife have dual marriages, I mean, married in each dual country, itakuwaje