Mjamzito kulala chali kuna tatizo?

henya

Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
62
Reaction score
25
Habarini za asubui!

Mimi ni mjamzito wa miezi sita, nikilala chali naskia kama mtoto anapanda kifuani. Je, hili ni tatizo? Au hairuhusiwi mjamzito kama mimi kulala chali?
 
Haishauriwi kulala chali mama mjamzito kama nakumbuka yaweza sababisha shock, Pathophysiology nimesahau, has been a while wataalamu zaid wataweka sawa.
 
Sio vizuri bi dada mara nyingi hileta matatizo ya kubanwa.na pumzi mana mtoto hufanya kama kupanda mpaka kwenye chembe cha moyo. Lkn sijui kwa nn inakuwa unajiskia ham sana kulala chali. Mi mwenyewe now nna ya miezi minne basi nkilala chali najiskia kama resting flan ivi.

Ila kadri mtt akikua sio advisable.
 
wanasema pia ukilala chali mfuko wake wa hewa pia unaudisturb so naye anahangaika
 
Wanasema mzunguko wa damu unakuwa auendi vizuri maana uzito wote wa mwili unakuwa unahamia mgongoni na inaweza kukusababishia maumivu ya mgongo ,low presha na kukufanya usikie kizunguzungu.

Best sleeping position weka mto katikati ya mapaja na mwingine nyuma ya mgongo utapata supoti nzuri tu.
 
Mgongoni kuna mshipa mkubwa wa damu unaorudisha damu kwenye moyo - inferior vena cava.

Ukilala chali mtoto anaweza kukandamiza mshipa huu. Matokeo yake damu toka miguuni na tumboni hairudi kiasi cha kutosha kwenye moyo.

Kwavile hairudi ya kutosha basi hata damu inayosukumwa na moyo kwenda sehemu nyingine za mwili pia inakuwa haitoshi.

Organ ya kwanza kufeel upungufu ni ubongo. Mjamzito ataanza kusikia kama kizunguzungu, mwili unapoteza nguvu na anaweza kupoteza fahamu.

Damu anayopata mtoto pia inapungua na iwapo mtoto hana "reserve" ya kutosha, hali hii inaweza kumuathiri.
 
Sory ina maana hata ukitaka kufanya mavituz huruhusiwi kulala chali!!??
 
Kulala chali kwa mjamziti ni hatari kwa mtoto?
May 12th, 2013 · 0 Comment
Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali -wapo kwenye hatari -ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi.

Katika utafiti -uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito -walikuwa -kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na -kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.

Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu.

Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya -watoto wafu wanaozaliwa -katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

Mkuu wa utafiti huu,Louise O'Brien -kutoka chuo kikuu cha Michigan, nchini Marekani amesema kama kutokulala chali wakati wa ujauzito hupunguza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu basi ni vizuri kuhamasisha kina mama wajawazito kutolala chali kwani hii ni njia rahisi na isiyokuwa na gharama yoyote ile.

Tabia hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa kuwashauri -kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala chali.

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watoto wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya kulala tu kwa wanawake wajawazito.



Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.

Utafiti huu uliofanyika nchini Ghana unaunga mkono utafiti uliofanyika hivi karibuni nchini Australia unaojulikana kama Sydney Stillbirth Study ambao ulisema ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito wako kwenye hatari ya mara sita zaidi ya kuzaa watoto wafu.

Utafiti huu wa Australia ulifanyika kwa miaka mitano na ulihusisha wanawake wajawazito 295 kutoka katika hospitali nane nchini Australia. Naye mtafiti mkuu katika utafiti huu Dr. Adrienne Gordon, kutoka Sydney's Royal Prince Alfred Hospital amesema "Tafiti za awali zilionyesha ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito, hupunguza mzunguko wa damu unaotakiwa kwenda kwa mtoto.

Lakini -pia ni vizuri kwa wanawake ambao ni wajawazito -kutotaharuki kama wakati mwingine watalala chali.''
Kutokana na idadi ndogo ya wanawake wajawazito waliohusishwa kwenye utafiti huu sisi wana Tanzmed tunachelea kusema ya kwamba ni vigumu kusema utafiti huu umetoa mapendekezo sahihi ya -namna ya kulala kwa wanawake wajawazito.

Pia kutokana na kutoangalia muda ambao wanawake hao walilala wakiwa chali (mfano kama walilala masaa 4,6 au 8 kwa siku na kwa siku ngapi) na tofauti ya hatari kati ya wanawake wajawazito waliolala muda mfupi na mrefu, hivyo tunawaambia wanawake wajawazito kutohofu kama watalala chali lakini ni bora kuchukua tahadhari mapema.Tafiti hii inatoa changamoto kwa watafiti wetu wa afya kuangalia jinsi ya kufanya tafiti kama hizi katika mazingira ya kwetu.

Source: dullonet.com/afya/kulala-chali-kwa-mjamziti-ni-hatari-kwa-mtoto/
 
Kwa hiyo walale kifudi kifudi au huu ndo uwongo wwnyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…