Mjane anapataje haki kutumia akaunti za Marehemu Mumewe?

Mjane anapataje haki kutumia akaunti za Marehemu Mumewe?

Mbikiboy

Member
Joined
Feb 15, 2019
Posts
89
Reaction score
86
Wadau kama nilivyoandika, kaka yangu alifariki mwezi wa tano mwaka huu. Sasa mjane ndio ameteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi baada ya kikao cha familia. Utaratibu ukoje ili aanze kutumia akaunti za marehemu ukizingatia ana shida ya pesa.
 
Anatakiwa awasilishe nyaraka na barua za mahakamani zinazomtambua kama mrithi wa mirathi ya mwanaume wake.

Swali la kizushi anapokufa mwanamke huwa kunakuwa na mjadala wa mirathi ya mali za mke?!
 
Mjadala utakuwepo kutegemea na mchango wa mke katika ndoa husika.

Anatakiwa awasilishe nyaraka na barua za mahakamani zinazomtambua kama mrithi wa mirathi ya mwanaume wake.

Swali la kizushi anapokufa mwanamke huwa kunakuwa na mjadala wa mirathi ya mali za mke?!
 
Mjadala utakuwepo kutegemea na mchango wa mke katika ndoa husika.
Swala sio mchango. Tuseme mimi nimekutana na binti ana nyumba tayari tukafunga ndoa tukajenga yetu ile yake tukapangisha.... Au tukapangisha yetu tukaenda kukaa yake, je hapo imekaaje kwenye swala la mirathi?!
 
Hiyo nyumba kisheria baada ya ndoa ni yenu wote kwa hiyo wewe cha kufanya ni kufuata sheria ili ubadili Title deed iwe na jina lako tu. Sheria za Tanzania kwenye mirathi zina miaka chungu nzima sijui kama nilichoandika kiko sahihi. Na hapo tuna assume nyumba ya mke ilikuwa yake pekee kabla hamjaoana.
 
Aende bank na death certificate, pamoja na resolution ya familia kumteua msimamizi wa mirathi then atapewa utaratibu unaofata
 
Anachotakiwa kufanya ni kufungua shauri la mirathi mahakamani ,mahakama itatoa tangazo la siku za 30 kwa anayepinga kisha shauri litasikilizwa akiwa na mashahidi ambao ni ndugu wa marehemu baada ya uteuzi mahakama ndio itayoindikia bank taarifa kuwa wafunge account ya marehemu kisha fedha zitawekwa account ya mahakama iliyoko bank kuu.

Baada ya hapo warithi halali wa marehemu wataganywa hicho kiasi cha pesa ambacho kitaingia moja kwa moja kwenye account ya mrithi halali yaani watoto na mjane wataanza kuwapa watoto wadogo kiasi kingi kisha ndo wengine watafuata
Mbikiboy
 
Back
Top Bottom