Mjane na ujumbe wa simu

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2016
Posts
202
Reaction score
145
Mzee mmoja alifika kijiji fulani akakuta mtandao wa simu unashika vizuri. Akaamua kumwandikia mke wake ujumbe mfupi wa maandishi aliyekuwa amemwacha mjini.

Bahati mbaya alikosea nambari akatuma kimakosa ule ujumbe kwa mtu mwingine ambaye ni mwanamke mjane aliyekuwa kapoteza mumewe siku za karibuni.

Mjane huyo alipokea ujumbe ili ausome maana bado watu walikuwa wanamtumia ujumbe wa kumfariji kutokana na msiba. Aliposoma ujumbe palepale akazimia!!

Mwanaye alipoona vile akausoma ule ujumbe ambavyo ilivyoandikwa:

“Mke wangu mepenzi najua utashangaa kuona SMS yangu kwako. Kumbe hata huku nako mtandao unapatikana kwa huko. Nimefika salama na matayarisho ya wewe kuja yamekamilika hivyo jiandae haitofika wiki ijayo na wewe utakuwa umeshanifwata huku''

Mtoto naye palepale chaliiii, akazimia.

Hata mimi nimezimia hapa
 
mamimi huku chali!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…