Mjapani: Inakuwaje watanzania zaidi ya milioni 50 mnashindwa kubangua korosho na kulazimika kuiuza kama malighafi?

Mjapani: Inakuwaje watanzania zaidi ya milioni 50 mnashindwa kubangua korosho na kulazimika kuiuza kama malighafi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Yule rafiki yangu injinia kutokea Japan ameshangazwa na taifa kubwa kama Tanzania lenye watu zaidi ya milioni 50 kushindwa kubangua korosho.

Mjapani ameniambia kuwa nguvu wanayoitumia wanasiasa kuongea kwa mdomo wangeishusha kwenye mikono yao taifa hili lingepiga hatua kubwa.

Yaani unauza korosho kwa bei sawa na 15% ya bei yake halisi kwenye soko kwa sababu ya " uvivu" tu wa kuibangua? Hyo kule Japan au Korea ya kusini na China isingewezekana.

Watanzania wamewekeza zaidi kwenye kuongea badala ya kutenda. Endapo watabadilika na kuwa watendaji zaidi kama Rais Magufuli anavyowabadilisha, basi wanaweza kuufikia uchumi wa Korea Kusini au Singapore na kuupita.

Hii ni habari njema kutoka kwa rafiki yangu Mjepu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ila nimecheka sana na hoja yako ndugu John
 
Sio walaji je. Kopo hilo $15.
1572615327094.jpeg
1572615374083.jpeg
 
Mwambie mjapani atusaidie kuitoa CCM madarakani hatokaa ashange jambo lolote nchini, CCM ndio tatizo mwambie.
 
Tatizo sio watu milion 50, tatizo ni mfumo wa uongozi uliopo. Bila kuweka mfumo wa uongozi unaoweza kujiendesha wenyewe, hata aje Putin tutaendelea kuuza raw products. Kiongozi anatakiwa abakie kuwa msimamizi wa watenda kazi, sasa hapa kwetu ni kinyume chake.
 
Sera ya viwanda bado haijanyumbulishwa,ili kuleta uwanja mpana wa ushiriki wa mwananchi na mwekezaji yoyote kutoka popote duniani ili kuwekeza katika viwanda.
 
Back
Top Bottom