MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Kumekuwa na mijadala mikali sana kuhusu nini kitangulie kwenye maisha ya mjasiriamali/mfanyabiashara, nyumba au gari? Watu wengi sana wamekuwa wakikatishana tamaa kwamba kununua gari kabla hujajenga ni upuuzi na uamuzi mbaya. Ni kweli wana sababu nzito kwasababu ukiachana na nyumba kukuondolea gharama za kulipa kodi ya kupanga lakini pia nyumba ni asset inayoeleweka na inaweza kukusaidia endapo utahitaji mkopo. Lakini pia nyumba inakuongezea thamani yako binafsi na kuaminika na wengi. Wenyewe wanasema ni muhimu kuwa na anwani mjini. Faida za kuwa na nyumba ni nyingi na zinajulikana. Lakini je, bado ni sheria kwamba tusinunue magari kabla hatujawa na nyumba?
Binafsi ninavyoona ni kwamba kama kuna uwezekano wa mtu kujenga nyumba kirahisi basi afanye hivyo bila kuchelewa. Ila kama gharama ya nyumba ni kubwa sana ninamshauri mjasiriamali asijitese kuanza kujenga huku bado biashara ikihitaji pesa nyingi kuweza kusimama vizuri. Kwa mfano mjini Dar es Salaam ukiwa na kiwanja basi hadi kukamilisha nyumba yako sio chini ya Tsh 50m.
Hapo kina ni kirefu. Mimi nashauri kwa mfanyabiashara ambaye bado hamudu hizo gharama basi anunue gari lake zuri na kulikatia bima comprehensive. Gari litampa utambulisho wa haraka kwenye jamii na wadau watajenga imani naye. Lazima ukiwa mfanyabiashara uonekane uko sawa hasa na taasisi za kifedha. Ikumbukwe taasisi za kifedha hazina urafiki wowote na mtu mwenye harufu ya umaskini.
Kuaminika mjini sio jambo la kitoto. Kuna michakato mingi inahusika. Wasanii huwa wanaita kuji-brand. Cha kuzingatia ni kuendelea kupiga kazi kama punda huku ukitumia vizuri imani uliyojijengea kwenye jamii. Usinunue gari kwa nia ovu. Wanawake wengi wanapoona mtu anaendesha gari huwa wanavutiwa nae mwishowe ni kijana kunasa mtegoni. Ila ukitumia gari kujiongezea thamani mbele ya wadau muhimu kwenye circle yako basi utazivuta pesa zije upande wako.