Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Watanzania wamesikia kauli ya mkoa wa Dar, Albert Chalamila kuwa, mjawazito atawajibika kuchangia matibabu na akishindwa aende akajifungulie nyumbani. Japokuwa imetolewa kwa kebehi lakini ni kauli iliyobeba uzito mkubwa ikizingatiwa sera rasmi ya serikali katika sekta ya afya ni mjawazito kupatiwa huduma zote za msingi za uzazi bure ikiwemo kujifungua.
Sasa ili kuepusha migongano baina ya wanachi na watoa huduma, mamlaka zingine za kiserikali (za juu au kisekta) ni vyema zikaja hadharani kufafanua matamshi hayo kama ndio msimamo rasmi wa serikali kwa sasa kiujumla au kukanusha kauli ya Chalamila.