Mje mtushauri vijana wa miaka 25 hadi 40

Mje mtushauri vijana wa miaka 25 hadi 40

Utawala2025

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2023
Posts
1,144
Reaction score
2,755
Habari,

Nimekuja na mada hii kwa wazoefu wa maisha mnaweza kutusaidia sisi vijana wadogo ambao tuko kwenye miaka 23 hadi 40.

Maisha yetu yamekuwa ni ya matarajio mengi sana lakini uhalisia wa hayo matarajio ni tofauti na tunavyofikiria au tulivyoahidi.

Umri umefika tumejikuta tuna wake, watoto na kazi au vitu vya kawaida ambavyo hatukuwa na mipango navyo labda tuseme tunaona tumefeli.

Tuliwaza kumiliki Nyumba Kali, Gari nzuri, kuwa na kazi yenye mshahara wa kutosheleza mahitaji maishani na ndugu lakini haijawa hivyo.

Kwa wazoefu wa maisha.

Tunaomba mtushauri kitu gani cha ziada tufanye hili tuweze kufikia lengo la maisha wakuu.
 
Shida yenu ubishi! Tukiwaambiaga mnasema tunawaonea gere sababu mnapendwa na mishangazi!

Tulieni vijana! Tuheshimuni tuwashauri yaliyo mema.

Mnahisi nyie ndio wa kwanza kupitia hizo stage kweli? Au mnadhani nyie ndio mmegundua utamu wa pombe na utamu wa lile tendo? Tumepita humo humo na sisi vijana, tukiwashauri kitu ni kwa kuwa tunakijua! Shida mnaona sisi tumelost kwahiyo hatuwezi waambia kitu.
 
Habari.

Nimekuja na mada hii kwa wazoefu wa maisha mnaweza kutusaidia sisi vijana wadogo ambao tuko kwenye miaka 23 hadi 40.

Maisha yetu yamekuwa ni ya matarajio mengi sana lakini uhalisia wa hayo matarajio ni tofauti na tunavyofikiria au tulivyoahidi.

Umri umefika tumejikuta tuna wake ,watoto na kazi au vitu vya kawaida ambavyo hatukuwa na mipango navyo labda tuseme tunaona tumefeli .

Tuliwaza kumiliki Nyumba Kali,Gari nzuri ,kuwa na kazi yenye mshahara wa kutosheleza mahitaji maishani na ndugu lakini haijawa hivyo.

Kwa wazoefu wa maisha.

Tunaomba mtushauri kitu gani cha ziada tufanye hili tuweze kufikia lengo la maisha wakuu
Msiishi kwa ajili ya watu wengine, ishini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu aliyewaumba.

Kwanza kabisa mnatakiwa na mnapaswa mueelewe kwanini mliumbwa mkawepo duniani?
 
mimi ni kijana ambae nipo katika umri huo, na ofcoz tumekua na matarajio mengi na tumefeli kuyafikia... cha kwanza mi bawashauri vijana muoe ingawa najua wengi watanipinga... ila kuoa kutakutoa wenge... cha pili vijana wengi hawana malengi yenye deadline... yan naweza akawa analwngo lakin hajua atalitimiza vipi na lini... cha tatu ni kujitenga na watu wanaoweza kukufanya usiwe karibu na vita dhidi ya ndoto yako... acha bata acha kuinjoy mana umeweka deadline hayo mambo utayafanya ukifikia shabaha yako
 
Habari.

Nimekuja na mada hii kwa wazoefu wa maisha mnaweza kutusaidia sisi vijana wadogo ambao tuko kwenye miaka 23 hadi 40.
Mada Nzuri mno.

Mpaka sasa Maisha yameendelea kuthibitisha kwamba hakuna “wazoefu/wataalamu juu yake, na haswaa sasa ambapo tupo katika kipindi cha mabadiriko ya Mfumo wa science & technology.

Binaadam wote ni wanafunzi wa Maisha wasiohitimu mpaka Umauti.

Maisha yetu yamekuwa ni ya matarajio mengi sana lakini uhalisia wa hayo matarajio ni tofauti na tunavyofikiria au tulivyoahidi.
Ni kujitahidi kwa dhati kuishi katika uhalisia wa wakati husika.

Kibaya zaidi matarajio ya sasa yameongozana na Matamanio bega kwa bega kiasi roho na nafsi ndio wahanga wakuu kupitia macho kuona.

Umri umefika tumejikuta tuna wake ,watoto na kazi au vitu vya kawaida ambavyo hatukuwa na mipango navyo labda tuseme tunaona tumefeli .
Somo kubwa jingine ambalo Maisha utufundisha kila siku ni kwamba, kilichopo ndani lazima kitaonyesha matokeo nje.

Na hakuna jambo litatokea bila dhamira ya muhusika kuwepo.

Tuliwaza kumiliki Nyumba Kali,Gari nzuri ,kuwa na kazi yenye mshahara wa kutosheleza mahitaji maishani na ndugu lakini haijawa hivyo.
Bado muda upo, kila sekunde ni nafasi ya uhai mpya kupitia pumzi mpya. Lolote linawezekana.

Kwa wazoefu wa maisha.

Tunaomba mtushauri kitu gani cha ziada tufanye hili tuweze kufikia lengo la maisha wakuu
Tumeumbwa kwa ukamilifu uliotimia katika Utulivu.

Ushauri ni mzuri, lakini kila hitaji letu limetimizwa kwanza ndani yetu kupitia dhamira ya uumbwaji wetu.

Tukiurejea Utulivu na kuskiza kwa roho na nafsi zetu huku tukiupa Uhalisia kipaumbele na kuyatawala mazingira yetu, chochote kinawezekana.
 
Back
Top Bottom