Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MJELEDI WA ASKARI WA KIRUMI ULIOKATAA KUMCHAPA YESU KRISTO
Wasomaji wangu nimekuelezeni mara nyingi kuwa katika utoto wangu nikipenda sana kuangalia senema, senema za maana zinazoeleimisha.
Katika moja ya senema zinazoishi ndani ya ubongo wangu hadi sasa nimekuwa mzee ni ''Ben Hur the Story of Jesus Christ.''
Hiki ni kitabu aliandika Lew Wallace askari wa Union katika jeshi la Marekani wakati wa American Civil War (1861 - 1865).
Juu ya jina hilo Yesu Kristo utakutananae mara mbili tu katika kitabu na katika hii movie, mwanzo wake na mwisho.
Kisa kizima kinahusu dhulma aliyofanyiwa kijana wa Kiyahudi Ben Hur kutoka mji wa Judea aliyekamatwa na kufanywa mtumwa akapelekwa kutumika katika manowari za kivita za Warumi kama mpiga kasia.
Nikisema nihadithie kisa kizima tutakesha hapa.
Waigizaji walikuwa Charlton Heston na Stephen Boyd.
Chalton Heston akiwa Ben Hur na Stephen Boyd Messala.
Yesu utamuona akimpa maji Ben Hur wakati akisafirishwa kwenda katika msafara wa safari ndefu na watumwa wengine kwenda Bahari ya Mediterranean akatumike kwenye manowari.
Yesu akiwa bado kijana mdogo labda wa miaka 25 msafara unapita nje ya nyumba yao na kwa kumuonea huruma Ben Hur anampa maji akiwa kaanguka chini hajiwezi kwa uchovu na kiu.
Askari wa Kirumi anamwendea kutaka kumtia adabu Yesu Kristo.
Yesu ananyanyuka alipukuwa kainama kumpa maji Ben Hur na anamkabili askari wa Kirumi aliyevaa mavazi ya vita uso kwa macho bila hofu.
Askari hakuweza kunyanyua mjeledi wake kumpiga Yesu Kristo.
Mijeledi ina historia ndefu.