BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Na Bwanku M Bwanku.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema amewaeleza wanahabari kwamba Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa sana kwenye maeneo yao hivyo wao wana jukumu kubwa la kueleza mambo hayo kwa wananchi ili waweze kuelewa kwa kina nini kinafanyika.
Mjema amezungumza hayo leo Jumatatu wakati akitoa salamu za CCM kwa maafisa habari hao kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kikao kazi cha 18 cha maaafisa habari, mawasiliano na uhusiano wa Serikali yaliyofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
"Ifahamike kwamba Ilani ya CCM ndiyo inayotekelezwa ndani ya Tanzania hii, na sisi kama Chama tunafurahishwa na tumeona kazi kubwa ya Serikali hii inayoongozwa na CCM. Serikali hii imefanya kazi kubwa sana chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi. Hivyo Wanahabari wote mlio kwenye sekta mbalimbali nipende kuwakumbusha kwamba hatuna shaka mtakwenda kueleza mambo makubwa yanayotekelezwa na Serikali yaliyoko ndani ya Ilani ya CCM." Alisema Mjema.
"Kwenye maeneo yenu kuna mambo mengi na miradi mikubwa inatekelezwa ikiwemo miradi ya afya, elimu, barabara, maji na kadhalika, kazi yenu ni kwenda kueleza yale makubwa yanayotekelezwa kule kwenu". Alisisitiza Mjema.
Mjema alishangazwa na miradi kwenye ngazi ya mkoa na wilaya kutoelezewa ipasavyo na hivyo kuwataka maafisa habari hao kwenda sasa kuelezea vyema miradi hiyo na kusema kwamba CCM itaendelea kufuatilia kwa ukaribu zaidi kuona haya yanafanyika.
Kikao hicho cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano Serikalini kitadumu kwa siku 5 mpaka Machi 31 na ni cha muhimu sana kikilenga kupeana mikakati ya upashanaji wa habari wa kimkakati kati ya Serikali na wananchi.