Hii nimeisoma mjengwablog;
Nimepumzika Kuandikia Raia Mwema
Kwa wasomaji wa makala zangu,
Baadhi yenu mmeshangaa kutonisoma kwenye ' Raia Mwema' toleo la jana. Nawajulisha kuwa nimepumzika kuliandikia gazeti la Raia Mwema ili niweze kuwaongoza wenzangu tulioshiriki kuandaa gazeti la Gozi Spoti ( Halipo tena mitaani) kujipanga upya kwa kutumia uzoefu tulioupata.
Tayari nimeshamjulisha Mhariri wangu ( Raia Mwema) kaka John Bwire juu ya uamuzi wangu huu. Natumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati ndugu zangu wa 'Raia Mwema' kwa kunipa fursa ya kuandikia gazeti hilo. Nimekuwa nikiandika bila kukosa tangu toleo la kwanza. 'Raia Mwema', kama ilivyokuwa kwa gazeti la 'Rai', limenisaidia kuifikia jamii pana ya Watanzania. Nimetengeneza mahusiano mema na Watanzania wengi wa ndani na nje ya nchi. Katika muda wangu na ' Raia Mwema', nimejaribu kwa uwezo wangu wote kuitumikia jamii yetu kupitia kalamu yangu. Nami nimejifunza mengi kupitia wasomaji wa gazeti hilo.
Naam. Nimepumzika. Kwa sasa nitabaki kuwa msomaji wa ' Raia Mwema'.
/Maggid