Mjerumani Afunga Ndoa Na Paka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Mjerumani Afunga Ndoa Na Paka

Tuesday, May 04, 2010 2:44 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani amefunga ndoa na paka wake kipenzi baada ya madaktari wa wanyama kumwambia kuwa paka wake ambaye ni mgonjwa hana siku nyingi atafariki. Gazeti la Bild la nchini Ujerumani limeripoti kwamba Uwe Mitzscherlich mwenye umri wa miaka 39 aliamua kufunga ndoa na paka wake baada ya kuambiwa kuwa paka wake huyo ambaye ni mgonjwa hana uhai mrefu.

Gazeti la Bild liliripoti kuwa Uwe alimlipa msanii euro 300 (Takribani Tsh. 540,000) ili aigize kama afisa wa kufungisha ndoa kwenye sherehe aliyoiandaa kwakuwa ni kinyume cha sheria kufunga ndoa na mnyama nchini Ujerumani.

Uwe alisema kuwa alitaka kufunga ndoa ya kweli na paka wake anayeitwa Cecilia kabla hajafariki kutokana na ugonjwa wa asthma.

Uwe ameishi na bi harusi wake ( paka wake) kwa zaidi ya miaka 10.

"Cecilia ni myama muaminifu, tunakumbatiana kila wakati na siku zote amekuwa akilala kwenye kitanda changu", alisema Uwe ambaye ni mfanyakazi wa posta katika mji wa Possendorf akiliambia gazeti la Bild.

Msanii Christin-Maria Lohri, ambaye ndiye aliyefungisha ndoa hiyo alisema "Mwanzoni nilifikiri ananitania lakini baadae niligundua kuwa Uwe alikuwa hatanii na hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake aliyokuwa akiisubiria iwe kweli".
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4431510&&Cat=2:angry:
 
So, atakuwa kisha mshuhulikia sana huyo paka mpaka ndoa!...
 
mi nahisi hawa wenzetu dhambi zaao hata shetani hazijui, lakini sijui inakuwaje magonjwa ya ajabu kama ukimwi hayawashughulikii ipasavyo kama huku kwetu ambako naona at least bado kuna morals. anyway i dont need to be a judge. let him (God )judge his people.
 
mwozeshaji na mwoaji wote wana tatizo fulani vichwani mwao. Hata hivyo yawezekana huyo alieolewa si paka bali ni shetani/jini katka umbo la PAKA.
 
Nadhani na kuamini kuwa sasa wanadamu ndio wanaomfundisha SHETANI dhambi kwani zingine hazijui kabisa anakuja kuzionea ktkt sayari hii.
Kaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaazi kweli-kweli
 
Nasikitika kusoma habari hii!!

Mungu yahurumie macho yaliyosoma habari hii
 
mwozeshaji na mwoaji wote wana tatizo fulani vichwani mwao. Hata hivyo yawezekana huyo alieolewa si paka bali ni shetani/jini katka umbo la PAKA.
mmh jamani shetani atakimbia dunioan mwaka huu manake mh.....kuna mengi ye hayajui...mungu aje tu afunge sayari yake......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…