Mji gani unafaa kuwa Center ya Sanaa Tanzania?

Paschal Ruta

Member
Joined
Jul 16, 2016
Posts
42
Reaction score
27
Ningekuwa na mamlaka husika ningechagua mji mmoja ambao ungejengewa miundo mbinu mbalimbali halafu wadau mbalimbali wa sanaa wakapewa motisha ya kuwekeza sehemu hiyo.

Katika mji huo kutakuwa na studio mbalimbali za production, studio za muziki, makampuni ya usaili wa wasanii, makampuni ya kuuza na kukodisha vifaa, vituo vya mafunzo, nk.

Kwa mtazamo wako unadhani mji gani ungefaa kwa jukumu hili? Inabidi kuzingatia mandhari ya eneo, hali ya hewa, mahali mji ulipo na ukaribu wake na miji mingine ya kimkakati, nk.

Ukishawekeza kwenye mambo ya msingi, kutachochea ujenzi wa mahoteli, migahawa, kumbi za starehe, makazi bora, nk.

PS. Dar es salaam na Dodoma hapafai.
 
Ila ukitizama sana pengine Dar maana ndo wasanii wote wanandoto ya kuja Dar, na sanaa zao
 
CHATO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…