Mji kasoro bahari Morogoro

Mji kasoro bahari Morogoro

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
MOROGORO IMEKOSA NINI?
Swali la dhati kabisa kujiuliza?
Magwiji wengi kwenye fani za siasa,michezo na muziki
MORO JAZZ BAND MBARAKA MWISHEHE aliiweka kwenye ramani Morogoro

Achana na BIFU la AFANDE SELE na PHILIP NYANDINDI A.K.A OTEN bifu la kugombea Ukubwa au ujogoo wa mji wa MJI KASORO BAHARI.

Bifu lililomalizwa kwa wimbo bomba unaoitwa TUSAHAU ft Suma lee
"mimi na wewe kumbuka ni kitu kimoja/
Wote tumetoka moro mkoa mmoja. ×2
Tusahau,yote yaliyopita/
Na tugange,yote yanayokuja/"×2

Kwa upande wa Muziki Moro imetoa wasanii wenye kukonga moyo haswaa na kifupi Moro HAINA KOSA HATA KIDOGO

Kwenye mziki wa kizazi kipya ukiacha ukubwa wa AFANDE SELE na watu pori, OTEN, Stamina ,Belle 9 ni nani amevuma ndani ya Moro na TZ nzima, Mkazi wa Moro Share na sisi tupate kuwafahamu wasanii wengi kutoka MJI KASORO BAHARI

AFANDE SELE KAELEZEA MJI WAKE VIZURI KWENYE WIMBO HUU HAPA CHINI

AFANDE SELE - NIKIWA MBALI ( MOROGORO)

Chorus.. ( MC KOBA)

Mwezenu mimi natoka morogoro/ najivunia kwetu mji kasoro Bahari/lazima nitarudi hata nikienda mbali/KWA vile ndugu zangu Moro wananisubili/ × 2

Verse 1.. ( Afande sele

"Amakweli mtu kwao kona zote za moro na mashabiki kibao/ ndio maana mimi ninaApa Popote nitapokwenda lazima nirudi hapa/ moro sifi na njaa hata mfukoni niwe kapa/ninapokuwa safari nikiwa kwenye treni/ ama nipo Ndani ya Gari/ ninapofika karibu naiona Moro kwa mbali/ imepapwa na milima/maji yanatililika utapenda kuyatazama/ japo sasa sio mengi tofauti na hapo nyuma/ Enzi za Baba mkwe wangu mlanzi Bado anasoma/ Ooh ilikuwa no ma hata kama kiangazi mtoni unaweza zama/ sasa hakuna Tena yote sababu wajinga wajinga mlima wanachoma/na Apa Haki ya mama kama unachoma mlima mpumbavu kila ukiema/ sababu hauna akili uelewi hii milima ndio mali zetu za Asili/ lakini ki usalama kidogo moro so shwari/ ki vipi subili mdogo koba atakueleza verse ya pili..

Chorus.. ( MC KOBA)

Mwezenu mimi natoka morogoro/ najivunia kwetu mji kasoro Bahari/ lazima nitarudi hata nikienda mbali/KWA vile ndugu zangu Moro wananisubili / × 2

VERSE : 2 MC KOBA

Asante kaka sele kwa kunipa nafasi/ namimi niseme ukweli/ ni kweli kiusalama kidogo moro sio shwari/ polisi wamezangaa mambo wanayofanya sometime mi na nashangaa/ ....
Wanakatama ndumu na baiskeli zisizo na Taa/ wakati majambazi wana nyaza kwenye mitaa/ na wale wana mgambo wanaotumwa na manispaa/ ni wafujaji wa fedha kwa mambo yasio kuwa na manufaa/ Enti wanavunja meza ya chinga kwenye mitaa/ wakati huduma muhimu kwenye jamii zimezupaa/ moro mji wangu mimi nieleze tu kipenzi/ unadhani una nuksi gani/ maanake hali Duni kwako wewe ndio nyumbani/ Kati ya watu sabini /hamisini ni masikini/ Uwezi kupata dili kama mjini ujulikani/ na labda usiwe na aibu/ ujipendekeze japo uwe karibu na waarabu/ ambao ni ndugu zetu toka Enzi za mababu/ wanatoka kule kule kilosa kilombero ifakara mpaka chakwaleee...

VERSE : 3 AFANDE SELE..

Afande sele ukipenda mzungu wa roho/ na ukipenda baba Tunda,/ ntawakilisha Moro kila pembe nnavyokwenda/ ntatukuza mazuri na mabaya ntayaponda/ mfano kuhusu kilimo Cha mbogamboga matunda/ama kuhusu michezo haswa mpira wa kandanda/Moro inafanya kweli miaka rudi miaka nenda/ukitazama muziki Morogoro ndio nyumbani/ ilianza kushika chati miaka mingi hapo zamani/ enzi za mziki wa dansi ulipovuma kama upepo/ na sisi mpaka sasa tunatesa kwenye hip-hop/sijui tungekuwa wapi Mbaraka wa Mwishehe mpaka leo angekuwepo/ kama wewe ni mgeni ndio kwanza unafika Moro/ utakiri kweli mji na bahari sio kasoro/muulize Mc ndolo/watu tunajirusha tunajichanganya sawa na mwanza Dar Arusha/ viwanja viko vingi, jichanganye kokote mradi uwe na shilingi/ masela na mademu wanajirusha na madingi/vijana hawana hiyana/ mambo yote kupeana/ kunyimana hakuna maana/ mradi kabla ya kupona usikose kutinga zana/ ndio Moro ilivyo leo muulize Fred Kandeo, brother Kenny, K. O Samweli msuya mkama Deo/ radio station kibao/kwa upande wa salamu mabingwa wote tunao/ ukihitaji majina yao karibu Moro hii leo/ watu wanasemezana hewani kwa mitandao/ wengine wameshajaa kwenye nyumba za internet/ wanajifunza mengi mabaya na maendeleo.…

..Moro nyumbani nitarudi..... ×2

🔥🔥🔥🎶🎶🎶

#funguka...

Naombeni mnitajie kumbi za starehe zilizotamba sanaa Enzi hizo hapo mjini Morogoro..

Je? Ni kweli Moro Enzi hizo HAli ya kiusalama ilikuwa sio shwari..

Ukimtoa Selemani msindi a.k.a Baba Tunda " afande sale" ni msanii yupi mwingine aliyeang'aa kutoka Morogoro..
Follow page yetu Facebook ya UKWAJU WA KITAMBO kwa Mengi yanayohusu muziki wa kitambo
@everyone
+255767542202

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🎶
images-5.jpg
 
Back
Top Bottom