Papa Mopao
JF-Expert Member
- Oct 7, 2009
- 4,153
- 2,647
Huu mji ulikuwa maarufu sana miaka ya zamani pale Kiwira Coal Mines, zamani hapo palikuwa na ukumbi japokuwa haikuwa ya kisasa, ulijengwa kwa kutumia makuti, disco zilikuwa zinapigwa sana mle ndani watu kama kawa walizicheza sana mpaka vumbi mwili mzima.
Mji Mwema kulikuwa na makazi ya watu wa kila aina, ujirani ulikuwa na ladha ya aina yake, nyumba nyingi asilimia kubwa zilikuwa za makuti miaka hiyo kabla ya kujengwa nyumba za kisasa Block E na Block D kama sikosei, kulikuwa na Makazi ya Wachina kule juu mlimani tulikuwa tunapaita Msasani, sijajua chimbuko la Msasani ni nini pale kwa Wachina.
Kulikuwa na uwanja wa Mpira, Netball vyote vilikuwa jirani na Mji Mwema.
Hakika huu mji ulijenga utamaduni fulani wa Ujirani mwema kwa maeneo yote ya Kiwira Coal Mines miaka ya mwishoni mwa 80 hadi miaka ya 90 mwanzoni kabla ya kubomolewa na kujengwa nyumba za kisasa.
Kwa wakaazi wa Kiwira Coal Mines watakumbuka kwa huu mji