Mzee Muhidini Maalim Gurumo ni mgonjwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Wodi ya Mwaisela,wodi No.5.Mzee Gurumo ni mmoja wa wakongwe wa Muziki alianza Muziki mwaka 1960 akiwa na Bendi ya NUTA.
Muhidini anasumbuliwa na kujaa maji katika mapafu.Wapenda Muziki,Ndugu na Jamaa tupite Hospitali kumfariji.Sala na maombi yetu yaelekezwa kwake,Ili apate nafuu na kurudi katika shughuli zake za kawaida.
Amefanya kazi nzuri isiyo na kifani toka 1960. Hakuisaliti fani amepitia mabonde na milima, umri hauna huruma namuombea Mungu amtazame kwa karibu yuko mioyoni nwetu
Tuache maneno ohooo ananikumbusha sijui nini, Mungu amjalie, pls wana jamii hospital ni gharama mnaeno hayasaidii tufanikishe hata mchango wa fedha za matibabu zimsaidie mzee wetu.