Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Ponzi scheme inafanana na DECI tofauti yake yenyewe inafanyika kwa wawekezaji. Wawekezaji wa awali wanapata gawio kubwa ili kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi. Mpigaji wa kwanza anayetambulika kwenye mfumo huu ni Charles Ponzi na ndipo jina la Ponzi scheme lilipoanzia.
Benard Madoff ndie mtu aliyeendesha ponzi scheme kubwa zaidi duniani na kukusanya dola za kimarekani bilioni 20(hasara ya kwenye makaratasi ilifika $ bilioni 64) mpaka kupelekea kutoaminika kwa wall street, pia inatajwa kuchomoza kwa jina la Donald Trump kulianzia hapo. Madoff aliwaahidi ritani kubwa wawekezaji kwenye uwekezaji wao lakini walipowekeza Madoff aliingiza pesa hizo kwenye akaunti yake binafsi. Alilipa ritani hizo kwa wawekezaji wa awali
KUGUNDULIKA
Disemba 10, 2008 Madoff alimshirikisha kaka yake na watoto wake wawili kwamba kampuni yake ya ushauri wa uwekezaji ni utapeli na inakaribia kufilisika. Watoto wa Madoff ndio waliomchoma ambapo alikamatwa na vyombo vya usalama siku iliyofatia
HUKUMU
Mwaka 2009 hukumu ilitoka na kuhukumiwa miaka 150 jela lakini Madoff alifariki April 2021 akiwa na umri wa miaka 82.
WALIOWEKEZA
Zaidi ya watu 40,000 kutoka zaidi ya nchi 125 waliwekeza kabla Madoff hajakamatwa walikuwepo watu maarufu kama mshindi wa Nobel, Elie Weisel na muigizaji wa filamu, Kevin Bacon. Madoff alisema alianza utapeli mwaka 1990 baada ya soko kuganda kutokana na vita ya Ghuba
Wachunguzi wamesema Madoff hajawahi kufanya biashara yoyote na pesa hizo zaidi ya kuchukua pesa za wawekezaji wapya na kuwalipa wa mwanzo. Madoff aliacha taharuki kubwa kwa wawekezaji ambao tayari walikuwa washanyooshwa na mdororo wa kiuchumi uliotokea miaka hiyo.
MABADILIKO
Tukio la Madoff lilipelekea mabadiliko makubwa kwenye kamisheni ya soko la hisa ambao walishindwa kuona kwa miaka mingi wizi wa Madoff pamoja na tahadhari zilizojirudia ikiwemo kutoka kwa mpelelezi binafsi, Harry Markopolos ambae alisema ritani zinazotolewa na Madoff hazikuwa na uhalisia na zisingewezekana.
WAFANIKIWA KURUDISHA HASARA
Pamoja na hasara, kazi kubwa ilifanyika nchini Marekani kutafuta fedha zilizochukuliwa na Madoff na mpaka Nov 2022 kamisheni ilifanikiwa kulipa jumla ya $ bilioni 18.6 kwa wahanga 40,454 ambazo ni sawa na 88.35% ya hasara halisi walizopata.
KUFARIKI
Benard alifariki April 14, 2021 kwa ugonjwa wa ini akiwa anatumikia kifungo chake cha miaka 150(Kifungo cha juu zaidi kisheria. Watoto wake pia wote walifariki ambapo Mark Madoff alijiua mwaka 2010 na Andrew alifariki mwaka 2014. Dada yake Madoff na mumewe pia walikutwa wamefariki mwaka 2022 wakiwa na makovu ya risasi. Polisi waliirekodi kama mauaji/kujiua.
Ambao sio wapenzi wa maandishi wanaweza kumuangalia kwenye documentary iliyotolewa mwaka jana na netflix-The Monster of wall street.