Mjue binadamu mwenye sura mbili aliyeishi karne ya 19

Mjue binadamu mwenye sura mbili aliyeishi karne ya 19

Joined
May 29, 2020
Posts
30
Reaction score
24
EDWARD MORDRAKE BINADAMU MWENYE SURA MBILI ALIYEISHI KARNE YA 19

By Mfalme Mastories

NI vigumu kuamini lakini ndiyo ukweli ulivyo! Edward Mordrake ni Mwingereza mashuhuri wa karne ya 19 ambaye alijinyakulia tuzo za Nobel. Mordrake aliyetokea kwenye ukoo mashuhuri na wenye hadhi kubwa nchini humo, alitambulishwa zaidi kwa sura zake mbili, moja ikiwa kwenye uso wake wa kawaida na nyingine nyuma ya uso (kwenye kisogo).

Cha kushangaza zaidi inasemekana kuwa sura yake ya kisogoni haikuweza kula wala kuongea chochote na hata ikijaribu kuongea maneno yalikuwa hayasikiki lakini iliweza kulia, kucheka na kusikia kila neno.

Sura yake ya mbele ya uso imeelezwa kuwa ilikuwa ni nzuri na ya kuvutia (handsome). Watu waliomuona na kuzungumza naye, wanamsifu Mordrake kwa uzuri wa sura yake ya usoni na tabasamu lake, lakini balaa lipo kwenye sura yake ya kisogoni ambayo ni ya kutisha na inayofanana na sura ya “bibi kizee mchawi”.

Simulizi za wafanyakazi wa jumba la kifahari alimoishi Mordrake, zinatolewa kwa siri, ambapo zinaeleza hali ya maisha ya huzuni ya kijana huyo iliyosababishwa na miujiza na mabalaa yaliyoletwa na sura yake ya kisogoni.

Mara kadhaa aliwaomba madaktari wamfanyie upasuaji wa “kuing’oa” sura hiyo ya kishetani, lakini sababu za kitabibu zilizoonesha uwezekano wa yeye kupoteza uhai endapo atafanyiwa upasuaji huo, hivyo walikataa kufanya hivyo.
Akiwa na umri wa miaka 23, Mordrake aliaamua kujiua kwa kunywa sumu baada ya kuchoshwa na mikasa hiyo ya sura mbaya aliyoiita kuwa ni ya kishetani, mikasa iliyokuwa ikimtokea mara kwa mara hasa usiku huku akiacha wosia kuwa sura hiyo mbaya ifyekwe kisogoni kwake kabla ya kuzikwa ili isiendelee kumtesa huko kaburini.

Kulingana na hadhi ya ukoo wa Mordrake nchini Uigereza, historia ya maisha yake haikuweza kuwekwa wazi ili watu wengine wakajua maisha yake.

Baki na Mimi
by #kingmastories

FB_IMG_1594004304248.jpg
 
Ni hekaya tu sidhani kama inawezekana kwa kitu kama hicho kutokea!
Sijui wazungu wanatuchukuliaje sisi cha kushangaza matukio yooote ya ajabu ajabu hutokea kwao tu mara sijui mtu aliishi akafa akaja kuzaliwa tena sehem nyengine mara sijui kuna abiria walikuwa kwenye ndege miaka kibao ndege ilipotea baadae wakaja kutua uwanja ganj sijui wa ndege huko kwao kwanini idingekuja kutua jkn nasi tuuakiki haya matukio? Kila siku kwao tu?
 
Back
Top Bottom