Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Mpishi huyo wa Nigeria amekuwa mtu maarufu wa kitaifa baada ya kupika bila kupumzika kwa zaidi ya saa 90 na kuvunja rekodi ya saa 87 na dakika 45 iliyowekwa huko Rewa, India ya kati mnamo mwaka wa 2019 na mpishi wa India Lata Tondon
Hilda Baci amepika zaidi ya sahani vyakula 100 tofauti tangu alipoanza kwa kupika Alhamisi saa 15:00 GMT Alhamisi.
Wanasiasa na watu maarufu kama Wiz Kid, Burna Boy, na Tiwa Savage wameonekana wakimtia moyo kwa namna tofauti, pamoja na umati wa watu wanaotazama akipika.
Guinness World Records inasema inachunguza ushahidi kabla ya kusema ikiwa amevunja rekodi hiyo.
Ingawa hakuna maafisa wa shirika hilo walio katika eneo hilo la Lekki la Lagos, kamera za CCTV zimefungwa kufuatilia tukio hilo.
Baci, 27, awali alipanga kupika kwa masaa 96 - hadi saa 15:00 GMT Jumatatu, lakini umati uliojipanga nje ya eneo la tukio ukimshangilia unamsihi kufikia saa 100.
Ametengeneza maelfu ya sahani za chakula, ambazo zinatolewa kwa wageni walioalikwa.
Anaruhusiwa kuwa na msaidizi mmoja kwa wakati mmoja, na anaweza kupumzika kwa dakika tano kila saa
"Jaribio hili ni ushahidi wa nguvu ambazo vijana wanaweza kuonyesha kwa jukwaa sahihi na msaada," mpishi huyo aliiambia BBC News Pidgin kabla ya kuanza kipindi chake cha kupika mara kwa mara.
Baci anaonekana akionyesha dalili za kuchoka kimwili na anapoozwa kwa barafu kichwani na masaji ya miguu wakati wa mapumziko yake. Msaidizi wa matibabu pia anachunguza mwenendo wake wa kiafya.