Bravo Michuzi,
My brother in blood, I grew up with the guy, ni mmoja wa vijana makini sana waliotulia niliowahi kuwaona katika maisha yangu wakichacharika na maisha, wakati sisi tukienda nje kutafuta meli, yeye ni mmoja wa wale waliobaki home "wakisotea meli za nyumbani", yeye ninamuweka kundi moja na Kuo, Bob Rich, Choggy, Chris Phaby, Shebby, Franco, Gibbson, Ray Abdu, Marcochella, Wandiba, Gerry Kotto, na wengineo.
Kwa kweli ni heshima kubwa kwangu kumuona kwamba kati ya wale tuliosota sana na waya mkali enzi za Mwalimu, na yeye ni mmoja wa wale walio-make it, ninamuona Michuzi akihangaika, hasa enzi zile za Disco Toto YMCA, chini ya DJ Kali Kali na Nigger Jay, I mean sijawahi kusikia Michuzi amemuibia mtu wala kuvunja sheria za jamhuri, huyu ni role model kwa vijana wengi wa kisasa wasioelewa namna ya ku-struggle, na ninakumbuka zamani jinsi sometimes tulivyokuwa tunakwama yaaani umepiga picha kwake hela za kulipia huna, mkulu Michuzi atacheka tu na kukwambia kazana lakini atakupa picha zako,
Bravo michuzi, na Mungu akubariki mkuu uendelee na uhangaikaji wa maishaa maana bado mwisho, sio siri kuwa mafanikio yako ni mwiba kwa wengine, maana maoni hapa juu yanajisema yenyewe, weka pamba mkuu, hapo juu ni clear kuwa hakuna anyejua ulikotoka kimaisha na hasa background yako, wanafikiri na wewe ni mtoto wa kibosile,
Mungu Akubariki Bro, A luta Continua!