Kwa mtu kama yeye kuwa na blog ambayo kila mtanzania wa ndani au nje akiingia kwenye computer ndo stop ya kwanza ni achievement kubwa....guys let us learn to appreciate the efforts of .. binadamu siyo kiumbe kamilifu, ...Kwa kweli inasikitisha sana, pale ambapo kazi za wenzetu ni kuangalia negatives tuu..its sucks!
As FMES said, Michuzi ni role model kwa wale wote wanaotafuta from humble background, bila kuwa na my uncle au aunt kwenye systems. God bless you man
Mengi unayosema ni kweli kabisa ndugu yangu. Lakini, naona kuna tatizo katika hoja yako. Wengi wanaotetea kitu au
figure fulani hapa JF wanatumia hoja kama yako kimakosa, kwamba kwa sababu hakuna aliye kamilika basi tusikosoane. La hasha! Mfano rahisi ninaotumia ni huu: mtu akikukanyaga bahati mbaya barabarani halafu akaendelea zake bila kukuomba msamaha, kama hajakuona wakati kakuona, utamshangaa au utasema hakuna aliyekamilika, hakutakiwa aniniombe radhi? Kwa nini binadamu tuna utamaduni wa kuomba msamaha wakati wote hatujakamilika? Ni kwa sababu mapungufu ya binadamu sio kisingizio cha makosa.
Tovuti ya michuzi ilikuwa inanuka matusi. Watu manapekeleka habari za vifo vya mama zao, halafu mtu anaandika..'aaah mama mwenyewe anaonekana alisha ishi miaka 60, na mategemeo ya maisha Tanzania ni nusu ya hapo, kwa hiyo inatosha.' Michuzi nae anaposti! Anapiga picha na watu, halafu anawaposti, watu wanaanza harusi ya kuwamaliza. Ndio maana nilimchukia sana michuzi.
Halafu, hii hoja ya kusema Michuzi hakuwa na mjomba kumpigia mapande, hicho ni kitu kizuri sana. Lakini inanikumbusha Mkuu Pinda alivyo sema alivyo twaa ukuu wa mawaziri: mimi ni mtoto wa Mkulima. Nilicheka sana. Tanzania ndio tuko kwenye kizazi cha kwanza ambacho sio watoto wa Wakulima. Kizaza cha kina Pinda wote wakulima. Lowassa, Sumaye, Malecela, Warioba, Salim, Msuya, Sokoine, Kawawa, toka Waziri Mkuu wa Kwanza Nyerere, wote walikuwa watoto wa wakulima.
Najua hatuongelei siasa hapa. Lakini hoja yangu ni kwamba Michuzi kufanikiwa bila kupigiwa pande sio chunuka. Kizazi chake chote ni watoto wa walala hoi! Asilimia kubwa ya Watanzania ni masikini, na wanaorithi mafanikio na kupigiwa mapande ni wachache mno. We nitajie tajiri Bongo au mkuu yoyote ambae karithi au kupigiwa Pande. Ni siku hizi ndio watoto wa Wakuu wanapewa makazi na Ubunge wa kuchaguliwa kwa sababu Rais anajuana na Baba zao. Lakini sio kizazi cha Michuzi. Sijui unakubaliana na mimi?
Mwisho kabisa, nadhani Watanzania lazima tujifunze tabia ya kuvumilia kukosolewa!