Mjue James Hardley Chase, Mwandishi maarufu wa Vitabu vya Riwaya

Hakika huu ni uzi pendwa sana.. Lakini cha kushangaza wadau watapita kama hawahuoni vile! KUSOMA VITABU KUNAONGEZA MAARIFA NA AKILI.
Teknolojia imebadilika sana mkuu,hapa utawapata wale wakongwe tu,sasa hivi movies ni nyingi sana na unazipata kiganjani tu kwenye smartphone yako,ukimwambia mtu asome kitabu hakuelewi,sio vitabu vya hadithi tu hata elimu pia imehamia mtandaoni,yale mambo ya kuwa na mavolume ya vitabu ni outdated kabisa kwa kizazi cha sasa...
 
Namshukuru baba yangu alinifanya nisome novels nyingi za James Hardley Chase nikiwa naanza form one nilishangaa nakutana darasan na mwalimu wa kingereza aliyesoma novel 2 tu plays 2 tu na vitabu viwili 2 vya mashairi. Nikasema ugonjwa wa lugha ya english hautakuja kuisha kwa sera mbovu ya elimu yetu.

Coffin from Hong kong
Well nowmy pretty
Mission to Venice
It is just the matter of time
A can of worms
 
Bujibuji Simba Nyamaume umenifanya machozi yanitoke kwa kunikumbusha mbali sana miaka hiyo. Nimesoma vitabu vingi vya James Hadle Chase na kuangalia movies ambazo zilitengenezwa kupitia stories zake.
Nakumbuka vitabu kadhaa kama
1. Well now my pretty
2. Dead man tell no tales na vingine vingi zaidi ya 50.

Pamoja naye nilikuwa mpenzi wa watunzi kama
Agatha Christie, Robert Ludlum, Danielle Steele, Sidney Sheldon n.k

Miaka hiyo watu tulipenda kusoma na kuazimana vitabu. Ukija kwa waandishi wa ndani yes umenikumbusha akina. F. Topan, S. Bawji, Eddie Ganzel, Akajase Mbamba, na hao uliowataja hapo juu..

WAKATI UMEENDA WAPI? 😔
 
Hakika huu ni uzi pendwa sana.. Lakini cha kushangaza wadau watapita kama hawahuoni vile! KUSOMA VITABU KUNAONGEZA MAARIFA NA AKILI.
.......nashukuru Kwa Uzi , angalau na Mimi nimepata Cha kusimulia kidogo kijiweni......'knock knock who is he'…....
 
Nawezaje kusoma kitabu cha simulizi za kubuni kurasa mia 3 na kuzimaliza zote?
Nina gain nini?
Sema TU hauna hobby na novels.Kusoma vitabu nya Chase ni sawa na kuangalia movie,kuna Mafundo kadhaa na ni njia nzuri ya kuulisha ubongo .Nadhani mpaka sasa nimeshasoma tittles kana 25.Ni vile tu upatikanaji wake mgumu,ningesoma zote 90
 
Tyga by the tail ilifurahisha mno.Mara ya kwanza niliisoma nikiwa secondari,baadaye nikapita ubungo nikaiona nikanunua .Nimeshairudia mara kadhaa
 
Huu Uzi umenifanya nirudi kabatini kukagua tittles nilizonazo,nadhani vijana wameshazipoteza zingine .Zimebaki chache Hadi nashangaa
1-Well now,my pretty
2-Figure it out for yourself
3-Tiger by the tail
4-Knock knock, who's there?
5-Not my thing
6-A can of worms
7-The fast buck
8-Gold fish have no hiding place
 
Nimepitia vitabu vyake huyu jamaa ila siku hizi nasoma on-line zaidi
 
Mimi nakumbuka title iliyonisisimua inaitwa "You are lonely when you are dead "
Lakini nimesoma vitabu kama 40 hivi vya Chase
 
Upewe Maura Yako[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Sikumbuki kusoma novel za Chase, wacha nizitafute.
Binafsi nampenda John Grisham; nimesoma novel zake karibia zote.
 
A coffin from Hong Kong ndio novel yangu ya kwanza kuisoma
Nimesoma jumla ya novel 26

Wakati ule ile slang iliotumika kwenye uandishi inge kuaminisha kabisa kwamba ndugu muandishi ni mmarekani aliyekulia “uswahilini” ya marekani katika viunga vya Bronx

Uzuri wa novel za Chase ni fupi lakini zinakuacha na kiu muda wate hadi umalize kitabu
Zipo direct na rahisi kuzielewa haswa kama English yako ni dhaifu
 
Sema TU hauna hobby na novels.Kusoma vitabu nya Chase ni sawa na kuangalia movie,kuna Mafundo kadhaa na ni njia nzuri ya kuulisha ubongo .Nadhani mpaka sasa nimeshasoma tittles kana 25.Ni vile tu upatikanaji wake mgumu,ningesoma zote 90
Nampenda Sydney Sheldon
 
Usishangae kaka. Utamaduni wa kusoma vitabu huanzia nyumbani
Sure. Mzee wangu aliishia darasa la nne lile la zamani, lakini pale home alijitahidi kutengeneza home library iliyojaa vitabu lukuki.
Magazine kama National Geographic nilianza kuyazoea toka niko mdogo ndio maana Geography ni somo nililokuwa nalibonda balaa shule kutokana na hobby ambayo mzee alitutengenezea.
 
Kusoma vitabu kunachangamsha sana ubongo. Novel ikiwa inaelezea msichana mzuri sana, ni wewe unamuona kwenye ubongo wako. Movie ikielezea msichana mzuri, ni yule ambaye movie director amemuona ni mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…