Mjue Kanali Seif Bakari, ivumayo haidumu, asubuhi imekaribia

Sasa umkute mjukuu wake twitter anavyojifanya ametoka ukoo wa watakatifu kumbe ni hamna kitu. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
..kuna watu wameuawa Znz wakati wa utawala wa Shekhe Karume na mpaka leo haijulikani walipozikwa.

..baadhi ya wanaotuhumiwa kuwapoteza Wazanzibari wenzao ni Col.Seif Bakari pamoja na wenzake waliokuwa ktk vyombo vya ulinzi vya Znz baada ya Mapinduzi.
 
Nnauye alikuwa kwanza Mwenyekiti wa TANU Youth League( miska ya 70 mwanzoni), halafu mkuu wa Wilaya Bagamoyo halafu RC Singida. Katikati ya miaka ya 70 ndiyo alikuwa mwalimu wa siasa jeshini.
 
Mjukuu wake ana haki ya kwendesha maisha yake apendavyo.
Hayo semwayo kama ni kweli anatoa wapi moral authority ya kupoint fingure kwa watu ambao hawafikii hata 0.0001% ya alichokifanya babuye?
 
Use your brain mkuu,lets say babu yako akiwa" mwiz"i wewe mjukuu inakuhusu nini mpaka usiwe "police"?
Alaf Moral authority wewe unaielewaje?
Hivi unafahamu hivi vitu spiritually huwa vinaenda vizazi hadi vizazi au haufahamu ukiua na mwanao ataua tuu ipo hivyo kama sio mwanao basi katika damu yako yupo ataifanya hiyo dhambi.

Je mhusika ameshawahi hata kusema babuye was wrong maana asiwe busy kutoa vibanzi wakati kuna maboriti ya hatari kwenye macho yake.
 
“Fedha ya kichwa cha Malkia si yako na usiniulize, labda niulize juu ya hii (sh.) yenye picha ya kichwa chako.”
😀 nimecheka sana.... Alikuwa anajiamini sana.... Hawa tuliokuwa nao visiwani sijui kama wanaweza haya!
 
Kawaulize watu wa Zanzibar ndio watakupa majibu kama alikua poa. Jamaa kaua sana watu kihuni huni tu
Tatizo la hawa watu, wakiwa na watu wao wa karibu wanakuwa wakarimu na wacheshi sana. Mpaka ukiambiwa huyu jamaa muuaji unakuwa kama huamini.

Kwa sababu mimi nilivyomuona katika mazingira rafiki alikuwa mcheshi na mkarimu sana inakuwa vigumu kuamini aliua watu bila kituo.

Lakini sijawahi kumuona katika mazingira yake ya kikazi akiindoa mazingira rarfiki.

Hata Joseph Stalin kuna watu walisema alikuwa mtu poa sana, lakini kikazi alikuwa anaua watu kama nzi.
 
inatia mashaka sana,binadamu wana pande mbili ubaya na uzuri
 
Kikosi cha Usalama wa Taifa chini ya Kanali Seif Bakari, kilichopewa jina la Viwavi Jeshi, kilichofunzwa Ujerumani Mashariki kikaiva kwa mbinu za utesi na mauaji, kilipewa mamlaka ya kukamata, kutesa, kutia kizuizini na hata kuuwa bila mashitaka
Haya mambo kama ya State Research Bureau ya Iddi Amin, Go with him to where he sleeps
 
Kumbi na wewe Bujibuji kwenye historia umo !.
 

Where the hell is this book? Haya ni madini ya nadra kupatikana.
 
Na si lazima ujue kila Kitu Ndugu na ndiyo maana huwa mnaambiwa kuna ambayo mnapaswa kuyajua ila mengine hampaswi pia muwe mnayajua.

Cha kushangaza hakuna ukweli unaofichwa chini ya kapeti usijulikane. Nia hasa ni kujifunza ili kuelewa namna bora ya kuendesha maisha yetu kwa manufaa ya vizazi vyetu vyote.
Sio busara kukataa elimu maana gharama yake ni kubwa mno. Tutafeli kwa kufanya makosa yale yale ambayo wenzetu walifanya na yakawarudi mazima
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tabia za madikteta wote zinafana..na mwisho wao unakuwa wa ghafla
 
sasa mtu wa namna hii huwa kwanini inatengwa siku ya kumkumbuka badala ya siku ya kupiga viboko kaburi lake! wajerman hawajawai kutenga siku ya hitler kwa sabab hizi hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…