Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 761
- 1,464
Anaitwa Annora Petrova, alizaliwa Mei 5, 1991 mjini Portland, Oregon US, alikuwa ni mchezaji maarufu wa mchezo wa 'skating' kutoka US tangu akiwa bado binti mdogo tuu.
Mchezo huu unaochezwa zaidi katika mataifa yenye barafu Annora alianza kujifunza tangu mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 13 tuu, baadaye akawa anaitwa kushiriki mashindano mbalimbali makubwa tuu ya mchezo huo nchini humo akiwa bado na umri mdogo, alikuwa na uwezo mkubwa sana katika mchezo huo.
Siku moja mwaka 2008 wakati anajiandaa na fainali ya mashindano ya mchezo huo ya Crystal Classic Championship kwa vijana yaliyokuwa yanafanyika kesho yake, aliamua aingie mtandaoni na kuji 'google' jina lake mwenyewe aone, majibu aliyoyapata yalimshangaza.
Katika mtandao wa Wikipedia aliuona ukurasa wenye kila taarifa inayomhusu yeye, na taarifa zote zilikuwa sahihi bila kujua ni nani ameziweka, ajabu zaidi ni kwamba taarifa hizo zilisema kuwa kesho yake atashinda na kubeba kombe katika fainali hiyo ambayo ni kweli alikuwa anatarajia kuicheza kesho yake.
Katika taarifa hizo katika ukurasa wa mtandao huo kuliambatana na picha hiyo juu ikimaanisha kuwa huyo ndiye Annora, akaachana nayo, kesho yake kweli akashinda taji, na akawa anaipitia page hiyo kila anavotaraji kucheza fainali, na anakutana na taarifa kuwa atashinda, na ni kweli anashinda.
Nyingine kati ya taarifa hizo katika ukurasa huo uliokuwa unamuandika yeye zilisomeka:- "Annora Petrova ni binti mdogo mbinafsi ambaye anakwenda kukipata anachostahili" alishtuka!.
Annora hakujua kabisa ni nani anahariri ukurasa huo na kuweka taarifa sahihi kabisa hadi za utotoni? akaamua kuhariri nayeye kwa kuongeza 'Annoura ameshinda Olympic', baada ya hapo maisha yake yalianza kupata misukosuko, ubora wake katika mchezo huo ukaisha.
Hali hiyo ilianza kumfadhaisha Sana Annora, akaamua kwenda kushtaki kwa Wikipedia wenyewe juu ya ukurasa huo ambao kwa lugha nyepesi waweza sema kuwa ulikua unatoa taarifa sahihi za Annoura hata kabla ya kutokea, yaani kama kesho Annora atapata ajali basi ukurasa huo utatoa taarifa hizo leo, kabla ya ajali yenyewe.
Alipofika makao makuu ya Wikipedia alishangazwa na taarifa ya kuwa hawauoni ukurasa huo anaoulalamikia kuwa unatoa taarifa zake, haukuwepo yaani.
Maisha magumu kwake yaliendelea huku ukurasa huo ukiwepo kama kawaida, lakini akienda kwa Wikipedia wenyewe kufuatilia hawauoni kabisa. Baadaye ukurasa ulitoa taarifa, update kumhusu Annora kama kawaida, taarifa hiyo ilisema:-
"Annora Petrova ni yatima mdogo anayetia huruma, ambaye wazazi wake walifariki kwa ajali mbaya"
Alishangaa sana kuona taarifa hii, na wazazi wake wapo, hawajafa, ikabidi awape tahadhari wazazi wake kwani mara nyingi alikuwa kila akisoma taarifa mpya kuhusu yeye katika ukurasa huo, ilikuwa inakuja kutokea kweli katika maisha yake.
Aliwaonya wazazi wake lakini walipuuzia, siku chache Baadaye alipata taarifa kuwa wazazi wake wamepoteza maisha katika ajali mbaya ya gari hali iliyompa mshtuko Annora na kupelekea kulazwa katika hospitali ya Swiss.
Baada ya muda Annora alipona na kila kitu kikawa kinakwenda vizuri, aliendelea kufanya mazoezi ya mchezo wake wa skating hadi siku alipokuja kutazama tena ukrasa huo wa Wikipedia na kupata taarifa mpya tena iliyoongezwa kumhusu yeye.
Ukurasa huo ulisema:-
"Annie Petrova alizaliwa Mei 5, 1991 na kufariki Oktoba 24, 2010, alikuwa mshindi wa mchezo wa skating Amerika ambaye alikufa peke yake akiwa yatima kwasababu ya upumbavu wake"
Annora alistaajabu sana, bado taarifa hizo zilizokuwa zinaongezwa zilikuwa sahihi kwamba alizaliwa Mei 5, 1991, na jina lake la utotoni alikuwa anaitwa Annie, japo hakuna tu aliyekuwa analijua jina hilo zaidi ya familia yake tuu, yeye alikuwa anaitwa Annora, watu wote walikuwa wanamjua hivyo, kuhusu tarehe ya kufa je?.
Utabiri huo ulikuja kuwa kweli, Oktoba 24, 2010 Polisi nchini Jamhuri ya Czech waliukuta mwili wa Annora hotelini juu ya meza yenye kompyuta aliyokuwa anaandika barua kwa rafiki yake Cum Bree aliyekuwa mchezaji mwenzake pia wa mchezo huo. barua hiyo polisi hawajawahi kuiweka wazi.
Uchunguzi wa kesi ya Annora aliyefariki akiwa na miaka 19 tuu haujawahi kupata majibu mpaka leo, haijulikani ukurasa huo ulifunguliwa na nani, na vipi uwe unatoa updates zote kuhusu Annora hata zile ambazo zitatokea siku za mbeleni na ni kweli zinakuja kutokea kweli? Unsolved.
Written by Military Genius
Sent using Jamii Forums mobile app