Mjue Luteni Zachariah Hans Pope wa JWTZ

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,904
Reaction score
4,902
Kwa wale waliosoma History huyu ndiye Luteni Zachariah Hans Pope wa JWTZ alieshiriki Ktk jaribio la mapinduzi ya kumpindua baba wa Taifa mwl JK Nyerere 1982 akishirikiana na kina kapteni Eugene Maganga, Luteni vitalis Mapunda, Luteni Kajaji Badru, Captain Hatibu Gandhi(Hatty McGee), Luteni Mbogolo, Captain Christopher Kadego, Luteni Pius Lugangila.....maafisa usalama wakiongozwa na comandoo Mabere Nyaucho Marando waliwashambaratisha Kabla hawajawampindua Nyerere.....inasemekana baada ya kukamatwa (isipokuwa Pius Lugangila alietoroka) walipelekwa ikulu na Nyerere alimkabidhi Hans Pope bunduki amuue ile awe rais yy Kama alivohitaji, Hans Pope alilia machoz na kugaragara chini huku akiomba msamaha, Nyerere aliwasamehe lkn walifungwa jela maisha, Hans Pope akiwa Gereza kuu Butimba ndie alieanzisha ligi kuu Gerezani huku akiunda timu ya Simba ya Gerezani......waliachiwa 1995 Wkt rais Ally Hassan Mwinyi akimaliza muda wake......kumbuka Hans Pope babake ni Mgiriki na mamake ni Mhehe wa Ipogoro lringa....ndo maana amekuwa akiidhamini Lipuli FC....


NIMEWEKA HISTORIA SAWA[emoji1547][emoji1547][emoji1547]
 
Mabere marando ni komandoo kumbe eh!!!!
 


Ukweli wa Jaribio la Mapinduzi Tanzania 1982 - JamiiForums
 
siku nyingine ukiwa unaandika vitu sensitive tuliza akili usiandike kama unakimbizwa
 
Pamoja na yote mi namkubali sana huyu Fieldmarshal [emoji109][emoji109]
 
Jf ina watu wenye upeo finyu zaid ya ufinyu wenyewe
 
very few facts patched up with a lot of made up stories
 
Babake hans pope alikua mkuu wa mkoa wa kagera na aliuawa katika vita ya Kagera 1978. ukiangalia ile video ya vita vya kagera wamesimulia na wameonyesha mazishi yake maeneo ya makanyagio Iringa. Babake Hasn pope ndo alikua na asili ya kijerumani pamoja na uhehe
 
Ndivyo ninavyojua. Ila wanasema aliuawa mwaka 1971, baada ya kutekwa na wanajeshi wa Uganda walipovamia Kagera kuja kuwatafuta wenzao waliokuwa wamekamatwa Tanzania.
Mwili wake ulihifadhiwa kwa siri hospitali ya Mulago toka 1971 hadi 1979 uliporudishwa Tanzania.
 

Samahani huyo Komandoo Mabere Marando ndiyo huyu huyu ninayemjua Mimi au labda ni Mabere Marando wa Jimbo linalogombaniwa la Idlib huko nchini Syria? Halafu hapo kwamba alikuwa Luteni mara sijui Nyerere alimpa Pistol ampige ili awe Rais Yeye na akagalagala huku akilia machozi nitakuwa wa mwisho katika Kukuamini. Na mwisho tu niseme kwamba kupitia huu Uzi wako sasa nimeamini rasmi kwamba kumbe Mtunzi Mahiri wa Hadithi nchini Tanzania siyo tu ' Ngosha ' Erick Shigongo. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Reactions: Pep
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…