Mjue mganga wa Diamond Platnumz

Mjue mganga wa Diamond Platnumz

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,039
Reaction score
5,560
Bila shaka kila mmoja anamfahamu kijana huyu kutokana na kipaji chake cha kuimba.

Hapa nitawafahamisha mganga wa Diamond Platnumz anaemfanya ang'are kila kukicha. Hivyo hivyo kila mmoja anatamani kujua Diamond Platnumz anatumia uchawi upi unaomfanya awe maarufu namna hiyo.

Bwana mdogo huyu amejizolea umaarufu chungu nzima kuanzia Tanzania na Afrika yote kiujumla.

Mganga halisi wa Diamond Platnumz ni juhudi, kujituma pamoja na uvumilivu, nyenzo hizo tatu ndio zimemfanya kijana huyo azidi kung'ara kila uchwao.

Bila kupepesa macho kijana huyo ndio msanii mwenye mafanikio makubwa nchi Tanzania na Afrika Mashariki katika upande wa muziki.

Ni aibu na kukosa maarifa kumfananisha na wasanii wengine ambao hajafikia hata robo ya mafanikio yake Diamond Platnumz amekuwa mbunifu, mvumilivu, juhudi pamoja na kujituma na ndio maana anazidi kuwa mcharo kila kukicha. Na huo ndio uchawi wa Diamond Platnumz.

Nimetizama ziara zake za hivi karibu alipo kuwa nje ya nchi kuanzia Sierra Leone na ile ya Guinea Bissau.

Kuanzia mapokezi mpaka kwenye shoo husika unagundua kabisa huyu jamaa sio wa kawaida.

Tizama yale mapokezi apata utadhani ni kama ameenda Tandale kumbe yupo Kaskazini na Magharibi mwa Afrika. Ukifika wakati wa shoo ndio balaa lenyewe sasa anawaimbisha vile anataka.

Kongole kwake, kama binadamu naye ana mapungufu yake.
 
Me nilijua kuna picha ya mganga
images.jpeg
 
Mkuu umenena vyema. Inaelekea wewe ni mfuasi wa falsafa ya Baconian Induction.
 
Huo ndio ukweli.......
Hata kama angekua ana mganga wa jadi....
Juhudi na uwezo kutoka ndani anavyooo...

Wewe mwenzangu na mm hata kiswahili huwezi unachapia na kiha, unaimba km unasoma kiarabu nani akuaguee?
Wewe ni wa kupigwa jini tuuu...
 
Dah we jamaa! Mi nkajua utatuwekea huyo mganga na contacts zake ili vijana tumiminike huko? Duuh umenikomoaje?
Nimeingia kwa pupa na kwa furaha nikijisemea "hapa nishatoboa" Loh! Ngoja nijiendee kuzimua ubongo na gongo mchachuo kwa mama mwafu...
 
The BOSS1, Nikajua mambo ya matunguri kumbe ni ushubwada tu. Ngoja niwe bize na fiesta me hapa uhuru stadium.
 
Kijana yupo vizuri Sana ila yawe mapokezi alitopata Sierra Leone sio poa kabisa mzee lowassa alikuwa anasema mahaba.
 
Aisee hizi heading za YouTube mkome kuzileta huku,uhu ni ujinga kabisa.
 
The BOSS1,
Kitu pekee ambacho kinafanya wasanii wa Africa hasa kizazi kipya wasiendelee zaidi na kutoboa kwenye mabara mengine ni kushindwa kuimba LIVE. Unalipa kiingilio chako unaenda kwenye show kusikiliza playback, inakuwa haina tofauti na kuangalia tv. Raha ya show uone msanii anapafom mwanzo mwisho kwasauti yake halisi. Drums, gitaa, keyboard, trumpets, na vionjo vinginevyo uone vinavyopigwa live (angalia shows za Churchill Kenya. Wanamuziki wake wanaimba live bila kutegemea cd) muziki wa live una raha yake. Sio "sema yeeeea, sema wowo, mikono juu, imba" yaani show nzima unalipa kiingilio badala msanii akuimbie, wewe ndio unamuimbia msanii😂😂
 
Bila shaka kila mmoja anamfahamu kijana huyu kutokana na kipaji chake cha kuimba.

Hapa nitawafahamisha mganga wa Diamond Platnumz anaemfanya ang'are kila kukicha. Hivyo hivyo kila mmoja anatamani kujua Diamond Platnumz anatumia uchawi upi unaomfanya awe maarufu namna hiyo.

Bwana mdogo huyu amejizolea umaarufu chungu nzima kuanzia Tanzania na Afrika yote kiujumla.

Mganga halisi wa Diamond Platnumz ni juhudi, kujituma pamoja na uvumilivu, nyenzo hizo tatu ndio zimemfanya kijana huyo azidi kung'ara kila uchwao.

Bila kupepesa macho kijana huyo ndio msanii mwenye mafanikio makubwa nchi Tanzania na Afrika Mashariki katika upande wa muziki.

Ni aibu na kukosa maarifa kumfananisha na wasanii wengine ambao hajafikia hata robo ya mafanikio yake Diamond Platnumz amekuwa mbunifu, mvumilivu, juhudi pamoja na kujituma na ndio maana anazidi kuwa mcharo kila kukicha. Na huo ndio uchawi wa Diamond Platnumz.

Nimetizama ziara zake za hivi karibu alipo kuwa nje ya nchi kuanzia Sierra Leone na ile ya Guinea Bissau.

Kuanzia mapokezi mpaka kwenye shoo husika unagundua kabisa huyu jamaa sio wa kawaida.

Tizama yale mapokezi apata utadhani ni kama ameenda Tandale kumbe yupo Kaskazini na Magharibi mwa Afrika. Ukifika wakati wa shoo ndio balaa lenyewe sasa anawaimbisha vile anataka.

Kongole kwake, kama binadamu naye ana mapungufu yake.
Umemaliza mkuu. Ngoja waje akina yoh,watakutupia mawe
 
Back
Top Bottom