Mjue Mkata Umeme Halisi-N'Golo Kante

Mjue Mkata Umeme Halisi-N'Golo Kante

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Mjue N'Golo Kante a.k.a Mkata umeme
kante.jpg


Jina kamili; N'Golo Kante
Siku ya kuzaliwa; 29-March-1991
Miaka; 27
Mahali alipozaliwa; Paris, Ufaransa
Urefu; Meta 1.69 (Futi 5 na inchi 6½)
Nafasi; Kiungo mkabaji
Timu ya klabu; Chelsea
Jezi namba; 7
Timu ya taifa; Ufaransa
N'Golo Kante ambaye pia ana uraia wa Mali alianza maisha yake ya soka akiwa na miaka 8 katika klabu ya Js Suresnes ambapo alianza kuichezea mwaka 1999 mpaka mwaka 2010. Na baada ya hapo akaenda Boulogne mwaka 2010 mpaka 2011 na ndipo akapandishwa mpaka kikosi cha wakubwa ambapo alipandishwa mwaka 2011 na kufanikiwa kuichezea michezo 38 na kufunga magoli 3 kabla ya kuuzwa kwenda Caen mwaka 2013.

Caen ambayo aliichezea wakiwa ligi daraja la kwanza na kufanikiwa kuichezea mechi zake zote na mpaka kufanikiwa kupanda kuingia kwenye ligi kuu ya Ufaransa maarufu Ligue 1. Mpaka mwaka 2015 alipouzwa kwenda Leicester ambapo timu hiyo ya Caen aliichezea michezo 75 na kufunga magoli 4.

Usajili wake wa kwenda Leicester ulikamilishwa na skauti ambaye aliwai pia kusaidia usajili wa Vardy na Mahrez, Steve Walsh kwenda katika timu hiyo ya Leicester ambapo aliisaidia kubeba kombe la ligi kuu msimu huo huo.
gettyimages-528985688-1-2048x1536_3463124.jpg


Mwaka 2016 ndipo alisaini Chelsea kwa dau la £32 milioni (Paundi milioni 32) na kuichezea michezo michezo 27 mpaka sasa huku akiifungia goli moja alilofunga dhidi ya Man utd katika ushindi wa 4-0.
686385218-1206x602.jpg


October, 23 alicheza dhidi ya Leicester kwa mara ya kwanza akiwa Chelsea na kuisaidia Chelsea kuikandamiza timu yake ya zamani kwa magoli 3-0 na yeye Kante kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

N'Golo Kante ndiye kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu England kwa msimu wa 2016-17, Kante amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ufaransa kutwaa uchezaji bora tangu Thierry Henry afanye hivyo mwaka 2004.
ngolo-kante-pfa-player-of-the-year759.jpg



Mwaka Huu 2018, amenyakua KOMBE LA DUNIA

gettyimages-999726146.jpg

Usilolijua kuhusu Kante ingawa anaichezea Ufaransa lakini hajawai kuichezea timu yoyote ya vijana ya Ufaransa.

Kuna picha duka inayosamba kumuonesha Ngolo akiuza maji, ukweli ni kwamba huyu hajawahi hata kidogo kuishi Mali ina BINADAMU NI WAWILIWAWILI

fb_img_1532426165841-jpg.817237

Kante's parents migrated to France in the year 1980 from Mali.He was born in Paris in 1991. Kanté began his career at the age of eight at JS Suresnes in the western suburbs of the capital, remaining there for a decade.

Kante has never lived in Mali and at no time in his life sold pure water.

Seven things you didn't know about Chelsea star N'Golo Kante, including riding a push scooter to training and being a trained accountant

Mjue N'Golo Kante a.k.a Mkata umeme | Mashabiki wa Chelsea
 
Back
Top Bottom