Mjue Rais wa kwanza wa Malawi, Kamuzu Banda

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Hastings.jpg

Ninatambua kuwa jina la Kamzu Banda si geni miongoni mwetu hasa kwa wale wana historia. Leo nitajaribu kumuelezea kinagaubaga huyu mfalume wa Nyasa land na Malawi ya leo. Ni wazi kuwa ukisoma vitabu mbalimbali vilivyomwandika Kamzu Banda havitaji tarehe rasimi aliyozaliwa ijapo alizaliwa mwaka 1898 na tarehe ikadiriwa kuwa ni tarehe 25 mwezi wa tatu au nne. Hakuna uhakika wa tarehe kwa kuwa enzi hizo hakukuwa kunatunzwa kumbukumbu. Kamuzu Banda alizaliwa karibu na Kasungu, Malawi iliyokuwa wakati ule sehemu ya eneo lindwa la Afrika ya Kati ya Kiingereza (baadaye Nyasa land). Wazazi walikuwa Mphonongo Banda na Akupingamnyama Phiri.

Neno Kamzu maana yake ni mzizi kwa lugha ya Kichewa ambayo huzungumzwa huko Malawi. Na inasemekana alipewa jina la Kamzu kwa kuwa Mama yake alitumia dawa za miti shamba ili kuweza kupata uezo wa kushika Mimba ndiyo maana baadae Kamzu Banda alikuja kuongeza jina lake baada ya kubatizwa na kuitwa Hastings Kamuzu Banda.

Kama ilivyo kwa watafutaji wengine, Kamzu naye baada ya kukua alianza kutafuta maisha yake badala ya kuwategemea wazazi wake. Mnamo 1915–1916 Banda aliondoka kwao akisafiri kwenda Rhodesia ya Kusini (sasa Zimbabwe) na mwaka 1917 aliendelea na safari hadi Johannesburg Afrika Kusini alipopata kazi kwenye migodi ya Witwatersrand. Wakati ule alijiunga na kanisa la African Methodist Episcopal Church na hapo ndipo askofu wa kanisa lile aliona kipaji chake na akamkubali kwa masomo hapo kanisani. Mwaka 1925 Banda aliondoka kwenda Marekani. Alisoma kwa miaka mitatu kwenye Wilberforce Institute iliyokuwa chuo cha Kanisa la A.M.E. akaendelea kwa miaka miwili Bloomington, Indiana, kwa maandalizi ya masomo ya tiba.

Kutoka huko alikaribishwa kuhamia Chuo Kikuu cha Chicago alipokuwa msaidizi wa profesa wa lugha aliyetunga kamusi na sarufi ya lugha ya Chichewa, akajisomea historia akamaliza shahada. Kwa msaada wa wafadhili aliweza kuendelea kusoma elimu ya tiba kwenye Meharry Medical College huko Tennessee alipomaliza mwaka 1937. Kwa kurudi kwao kama tabibu alihitaji mtihani kufuatana na mfumo wa Uingereza, hivyo alihamia Chuo Kikuu cha Edinburgh alipopokea vyeti vya tiba na upasuaji mwaka 1941. Alianza kufanya kazi ya tabibu huko Uingereza katika miaka 1941-1951.

Ikumbukwe kuwa kwa kipindi kile waafrika wengi wenye uwezowalikuwa wakichukuliwa kwenda kusoma nje. Ukisoma historia inatueleza kuwa wazee wengi waliokuja kuongoza mapambano walisoma Ulaya wakiwepo Babawa Taifa Mwalimu Nyerere, Nkuruma, Mgabe, Kenyatta, Obote, Neto n.k Banda naye baada kukaa muda mrefu nje miaka ya 1945 alirudi Malawi na baadae kuanza harakati za ukombozi. Alipata ali kubwa ya kwenda kuwapigania Wamalawi hasa panda ya kuombwa kuhudhuria mkutano wa Pan-African Congress mjini Manchester.Aliombwa kuhudhuria mkutano huu kwa kuwa alikuwa ndiye msomi wa kiwango cha juu tokea Malawi.

Hamu ya kwenda kuwaondoa Wazungu Malawi iliongezeka baada ya kuombwa na Wafrika wengi hasa wa Ghana kuwa aende Malawi kuongoza harakati za kudai uhuru. Mwaka 1958 kwenye mkutano wa chama cha Nyasa land African Congress (NAC) alichaguliwa mara moja kuwa kiongozi wa chama hicho kwa kuzingatia uwezo wake. Alikuta nchi yake Nyasa land kuwa sehemu ya Shirikisho la Afrika ya Kati ambako walowezi wa Rhodesia ya Kusini walikuwa na hasira kubwa na kuendeleza ubaguzi wa rangi. Banda alipinga kuwepo kwa shirikisho hili.

Alizunguka nchini akiwahutubia watu na kudai uhuru wa Unyasa. Kutokana na muda mrefu wa kukaa mbali na nyumbani alihitaji wafasiri lugha maana alishindwa kutumia Lugha mama yake.Wananchi wengi walimfuata na hadi mwaka 1959 harakati za uhuru ziliongezeka kiasi kwamba serikali ilitangaza hali ya dharura. Banda alikamatwa na kuwekwa jela kwa miezi 11. Chama cha NAC kilipigwa marufuku lakini wanachama nje ya gereza waliunda chama kingine cha "Malawi Congress Party" (MCP) na kumtangaza Banda kuwa mwenyekiti ingawa bado alikuwa jela.

Wakati huo wanasiasa wa Uingereza walianza kukazia uhuru kwa makoloni yake. Kwa hiyo Banda aliachishwa gerezani kwenye mwezi Aprili 1960 akapelekwa London kwa majadiliano kuhusu uhuru wa nchi.Baada ya uchaguzi wa Agosti 1961 ulioleta kura nyingi kwa chama chake Banda alikuwa waziri wa ardhi na serikali za mitaa. Tarehe 1 Februari 1963 alikuwa waziri mkuu wa Nyasa land.Mwaka 1964 aliongoza nchi kwenye uhuru kamili. Banda aliamua kubadilisha jina kutoka Nyasaland kuwa "Malawi".

Historia ya banda ni ndefu na ni interested history, lakini ngoja nikupeleke kwenye hali ya Udikiteta wa banda. Inaelezwa kuwa banda naye aliingizwa kwenye vitabu vya madikiteta kama ilivyokuwa kwa Idd Amini Dada wa Uganda. Mwaka 1964 ndipo inapotajwa kuwa Banda alianza kuonyesha kuwa ni dikiteta baada ya kutofautiana na Baadhi ya mawaziri wake. Banda aliingia kwenye mgogoro na mawaziri wake kwa kile kinachodaiwa kufanya maamzi mengi bila kuwashirikisha mawaziri wake. Walilalamika juu ya Banda kutoshauriana nao akifanya maazimio hasa, kuendelea kwa uhusiano wa kidiplomasia na Afrika Kusini (iliyofuata siasa ya apartheid) na Ureno iliyotawala makoloni ya Msumbiji n.k.

Banda kwa hasira aliwaachisha kazi mawaziri wake watatu tarehe 7 Septemba. Mawaziri wengine waliwafuata wakijiuzulu wenyewe. Maandamano nchini yalifuata na wafuasi wa Banda walipigana na wandamaji hao ambao walikuwa ni wafuasi wa mawaziri. Mawaziri wengi waliondoka nchini. Wawili walijaribu kuingia pamoja na wanamgambo wenye silaha kutoka Msumbiji lakini walishindwa.

Mwaka 1966 ndipo Malawi ikawa jamhuri na Hastings Banda rais wake wa kwanza na chama cha MCP kilikuwa chama pekee cha kisiasa. Udikiteta wa banda inatajwa ulianza uoteshwa hapa.Mwaka 1970 alitangazwa kuwa mwenyekiti wa maisha yote wa chama cha MCP. Hatua hii ilifuatwa na Banda kutangaza kuwa rais wa taifa kwa maisha yake yote na Umoja wa vijana wa chama cha MCP ulihakikisha kukomeshwa kwa kila upinzani nchini uliojaribu kuleta fyokofyoko pamoja na vyombo vya dola .

Wamalawi wote walipaswa kumtaja Banda kwa jina la "His Excellency the Life President Ngwazi Dr. H. Kamuzu Banda" kwa kuongeza "Ngwazi" ambalo ni neno la Chichewa lenye maana ya "shujaa". Kutamka maneno ya ukosoaji dhidi ya rais ilikuwa hatari. Alitangaza mambo mengi kuwa marufuku Malawi, kwa mfano wanawake kuvaa suruali, kuonyesha magoti, wanaume kuwa na nywele ndefu au suruali fupi. Makanisa yalipaswa kutafuta kibali cha serikali, Mashahidi wa Yehova walipigwa marufuku. Wamalawi wenye asili ya Uhindi walipaswa kuachana na nyumba zao na kuhamia maeneo ya pekee katika miji. Magazeti, vitabu na filamu vilichunguliwa na wakaguzi wa serikali.

Banda alifaulu kutunza amani nchini wakati wa utawala wake lakini aliongoza kama dikteta. Mwaka 1983 mawaziri watatu wa serikali yake waliuawa. Kadiri dunia ilivyokuwa inabadirika Banda naye ALIKUJA NA MTAZAMO MWINGINE. Kwa mara ya kwanza Banda mwenyewe alianzisha majadiliano kuhusu kukubali vyama vingi nchini. Mawaziri watatu waliunga mkono hoja hii na mara moja rais aliachisha baraza lote la mawaziri akaita mkutano wa bunge na kuachisha wabunge wote. Mawaziri watatu walifungwa katika chumba bungeni na kupigwa. Mbunge mmoja aliingia katika chumba hchoi na kuwaona wakiteswa alikamatwa pamoja nao. Wote wanne walipatikana wamekufa katika gari la Peugeot lililopinduka. Serikali ilizuia kufunguliwa kwa majeneza wakati na mazishi yaliyotokea usiku. Walitangazwa kuwa wahanga wa ajali lakini baadaye ilijulikana waliuawa kwa kupiga misumari katika vichwa vyao kabla ya kuweka maiti katika gari na kulisukuma katika korongo.
1579530927293.png
Ukisoma kwenye website mbali mbali za Malawi utakutana historia kubwa ya Malawi. Lakini pamoja na historia inayomtaja Banda kama dikiteta lakini Wamalawi leo wanamuona Banda , BAKILI MULUZI na Bingu wa Mutharikakama ndio waliiletea maendeleo Malawi. Marais waliofuata baada ya hapoyaani Bingu wa Mutharika , Jocye Banda na Peter Mutharika bado hawaa taswira nzuri kwa Wamalawi kama walivyokuwa wanawategemea. Wiki ijayo nitawaletea uhusiano wa Marais Kamuzu Banda Vs Joyce Banda na Bingu wa Mutharika Vs Peter Mutharika.

Na Elius Ndabila

0768239284
 
Haya ndio yalikua majembe ya africa, mtu hachaguliwi kwa pesa zake bali uzoefu
 
View attachment 1328668
Ukisoma kwenye website mbali mbali za Malawi utakutana historia kubwa ya Malawi. Lakini pamoja na historia inayomtaja Banda kama dikiteta lakini Wamalawi leo wanamuona Banda , BAKILI MULUZI na Bingu wa Mutharikakama ndio waliiletea maendeleo Malawi. Marais waliofuata baada ya hapoyaani Bingu wa Mutharika , Jocye Banda na Peter Mutharika bado hawaa taswira nzuri kwa Wamalawi kama walivyokuwa wanawategemea. Wiki ijayo nitawaletea uhusiano wa Marais Kamuzu Banda Vs Joyce Banda na Bingu wa Mutharika Vs Peter Mutharika.

Na Elius Ndabila

0768239284
Jeshi la Malawi lilimlazimisha kusalimu amri baada ya kick samba ratings vikosi vya Malawi Young Pioneers (MCP) hivi ni sawa na vikosi hatari vya Umoja wa Vijana wa CCM. MYP walikuwa wanaogopwa kuliko jeshi na polisi kiasi kuwa kila mwananchi alimuogopa mwenzake kwani huwezi kujua kama ni MYP na ukidakwa hurudi kwenu maisha. Baada ya jeshi kuvipiga vikosi hivi vilivyokuwa na nguvu za kijeshi ndipo wananchi wakajiona wamepata Uhuru na Banda akawa mpweke hivyo kuruhusu mfumo wa vyama vingi. Baadhi ya mawaziri walikimbilia Tanzania akiwamo waziri wa sheria Chirwa na wengine.
Jambo moja kuu aliifanya Malawi kuwa nchi isiyo na wezi wala wahuni, haulazimiki kufungua milango ya nyumba au gari yako hata baiskeli iache nje utaikuta asubuhi, ila siyo sasa.
 
Huyu dikteta hana tofauti na mugabe,na savimbi walizitumia elimu zao kuzibomoa nchi zao badala ya kuzijenga hapa elimu aikuwakomboa walifanya mambo kama awajasoma vile
 
Mtu apatikanaye baada ya mzazi kwenda kutafuta mitishamba ataacha vipi kuwa dikteta.
 
Wakati tukiwa wadogo tuliambia Banda alikuwa daktari wa malikia, ili kutekeleza jukumu lake hilo ikabidi ahasiwe ili asije kumgegeda malkia na akapata ujiko wa kuwa mwafrika pekee kuwahi kumgegeda malkia. Je hili lina ukweli au stori tu za kwenye gahawa?
 
Kumbe hata haya tunayoyaona hayajaanza leo!?
 
Back
Top Bottom