Mjue Thomas Edison Mgunduzi wa balbu

Salahan

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
2,963
Reaction score
3,685

Thomas Alva Edison (11 Februari 1847 - 18 Oktoba 1931) alikuwa mvumbuzi mashuhuri na mfanyabiashara nchini Marekani. Aliboresha vifaa kama balbu ya umeme, mikrofoni na kugundua gramafoni. Utafiti na uvumbuzi wake ulihusu hasa mitambo ya umeme. Akajishughulisha pia na mtandao wa ugawaji wa umeme.

Edison alizaliwa katika familia ya Ohio kama mtoto wa saba akasoma miezi michache tu shuleni alipofukuzwa kwa sababu hakupenda kutulia na kusikiliza akafundishwa na mamake nyumbani. Aligonjeka mara kadhaa na tokeo moja ilikuwa ya kwamba kuanzia umri wa miaka 15 alikuwa karibu kiziwi.

Alipata kazi yake ya kwanza kwenye kampuni ya telegrafu. Kazi hii ilimwachia nafasi ya kujisomea na kutengeneza vifaa vyake vya kwanza. Alipokuwa na umri wa miaka 21 alitengeneza machine ya kuhesabu na kukadiria kura kwenye chaguzi.

1877 alivumbua mashine ya kushika sauti ikaitwa "phonograph" na kuwa mashine mama wa gramofoni.

Akaendelea kuboresha balbu ambayo hakuvumbua lakini hadi kwake balbu zilidumu muda mdogo tu; 1879 alifaulum kutengeneza balbu iliyotoa mwanga masaa 40 na baada ya miaka mitatu ya kuboresha balbu hii tena alifikia kwa masaa 1,000.

Edison alivumbua mengi; mapato kutokana na mauzo ya mitambo yeke yalimruhusu kujenga maabara makubwa na kuwaajiri muhandisi na wasidizi wengi.

Alitambua mapema ya kwamba kufaulu kwa mitambo ya umeme kulihitaji mtandao wa usambazaji wa umeme. Aliendelea kutengeneza swichi na mita ya kuhesabu matumizi ya umeme.

Tangu 1881 kampuni ya Edison ilianza kuweka waya za umeme mjini New York na 1882 alimaliza kituo cha umeme cha kwanza. Hadi 1911 kampuni yake ilkuwa na vituo 33 vilivyotoa umeme kwa balbu milioni 4.6 na wateja 108,500.

Kampuni yake iliendelea kuwa kampuni kubwa ya General Electric.

Ni mmoja wa watu maarufu na wavumbuzi wakuu, Thomas Alva Edison ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya maisha ya kisasa.



Alitengeneza vifaa vingi ambavyo viliboresha maisha duniani kote, ikiwa ni pamoja na santuri, sinema, kamera, taa ya umeme na simu.



Edison alikuwa mvumbuzi mkubwa na alipata hati miliki 1,093 za Marekani na nyingine nyingi Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani.

Uvumbuzi wake umechangia sana katika mawasiliano ya umma na, hasa, mawasiliano ya simu.

Mbali na kuwa mvumbuzi, Edison pia alikuwa mzalishaji bidhaa na mfanyabiashara.
Phonograph ya Edison ilikuwa machine ya kwanza iliyotunza sauti

balbu ya kwanza ya Thomas Edison iliyofanikiwa na kutumika
Menlo Park, December 1879

Thomas Edison katika tafiti zake za kugundua balbu inayowaka alijaribu materia tofauti tofauti elfu mbili(2000) ili apate iliyo bora zaidi kwaajili ya balbu. Baada ya material zote kutofaa kwa kuridhisha, msaidizi wake akaanza kulalamika kwa kusema “Kazi yetu yote ni bure kabisa,hakuna tulichojifunza”

Thomas Edison akamjibu kwa kujiamini sana na kusema, “Oh,Tumetoka na tafiti hii mbali sana na tumejifunza mengi.Tumejifunza na tumejua kwamba kuna material hizi elfu mbili(2000) ambazo haziwezi kutumika katika kutengeneza balbu iliyo bora.”


Nukuu: Usikate tamaa hata kama unajaribu mara kadhaa na kushindwa.



Mazungumzo juu ya Nukuu:

Mafanikio yako yanategemea ni mara ngapi umejaribu. Kufanikiwa pia kunategemea pia mara ngapi umeshindwa na kujifunza kutokana na makosa yako.

Thomas Edison ni mvumbuzi ambaye amefamika kufanya majaribio mengi sana na mengi katika hayo yalishindwa,lakini hakuacha. Aliendekea kujaribu mpaka pale alipofanikiwa.

Hivyo ukitaka kufanikisha jambo fulani katika maisha yako,basi thubutu kujaribu na hata kama utashindwa mara kadhaa,usikate tamaa jaribu tena na tena hatimaye utafanikiwa.

Katika kila jaribio unaloshindwa jifunze, ufahamu nini kilikukwamisha ili mara nyingine unapojaribu usikwame katika kizingiti kile kile.

Vikwazo vyote vinapoisha kinachobaki ni mafanikio.



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…