Mjue Tiffany Trump, mtoto wa rais mpya wa marekani

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,588
Reaction score
11,668
Tiffany Trump (23) ni binti wa Donald Trump kutoka kwa mke wake wa pili Marla Maples, mwigizaji wa zamani na nyota wa Televisheni.

Mrembo huyo ambaye amefuzu chuo kikuu hivi karibuni, alikuwa hana kawaida yakujitokeza sana kwenye kampeni za Donald Trump, lakini alisifiwa sana na baba yake kwa kutoa hotuba nzuri sana wakati wa kongamano kuu la chama cha Republican, ambapo alisema babake ni mtu mwenye sifa za kuwasaidia na kuwahimiza wengine.

Kwenye mitandao ya kijamii, Tiffany hupendelea sana Twitter na Instagram akiwa na wafuasi zaidi ya 236,000 na sifa yake kubwa ikiwa ni mara kwa mara kutuma ujumbe wa kifahari na picha zakuvutia.

Chakufurahisha zaidi ni kwamba mchumba wake anayetambulika kwa jina la Ross Mechanic (21), ni mwanachama wa chama cha Democrat na amekuwa akitoa ushirikiano sana katika kumnadi Hillary Clinton mpinzani wa Trump kwenye mitandao ya kijamii wakati wa kampeni za kuwania urasi wa Marekani.

Tiffany ni mwanamitindo mashuhuri ambaye amefanya kazi na wanamitindo wengi maarufu nchini Marekani kama vile Kya na Gaïa lakini pia ni mwimbaji mzuri ambaye aliianza kuimba akiwa na miaka 17.

Pampoja na mambo mengine Tiffany ni mtu mwenye kupenda marafiki na mwenye kupenda kushirikian na wengine katika mambo mbalimbali hasa yale ya kijamii.

Asenta.



 
Hii ni era ya wengi wasio na maarifa kuokota mapapai chini ya mnazi!


Urais siku hizi ni bahati nasibu, yeyote anashinda, Hata akizidiwa kura!


NINA USHAHIDI!
 
"Tiffany Trump (23) ni binti wa Donald Trump"

"mchumba wake anayetambulika kwa jina la Ross Mechanic (21),"




uwiiii mimi binafsi sipendi mwanamme anizidi AGE
Sasa kama una mwili wa kizee Mwanaume ukimzidi umri si ataonekana ni mwanao?

Hili ni jambo la kawaida sana huko mbelez, hata David Beckham amezidiwa mwaka mmoja na Posh Spice.
 
"Tiffany Trump (23) ni binti wa Donald Trump"

"mchumba wake anayetambulika kwa jina la Ross Mechanic (21),"




uwiiii mimi binafsi sipendi mwanamme anizidi AGE
problems zinaanzia hapa...

Mambo ya Nuh Mziwanda na Shilole kiuno
 
That's just you......and me! Lakini kwa wengine, age ain't nothing but a number!
Oops kumbe hupendi mwanaume akuzidi umri?? My bad, mm ni opposite, i like my man to be older even if it's just a liitle bit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…