Mzalendo_Mkweli
JF-Expert Member
- Jan 30, 2012
- 2,025
- 1,270
Tirunesh Dibaba, (alizaliwa Juni 1, 1985, karibu na mji wa Bekoji, mkoa wa Arsi, Ethiopia), ni mwanariadha wa mbio wa Ethiopia ambaye alishinda kwa mara ya kwanza mashindano ya dunia (World Championship) ya urefu wa 5000m akiwa na umri wa miaka 18 na siku 36 akielezewa kama “Youngest Ever Winner With Maturity Beyond Her Years”
Katika michezo ya Olimpiki ya Beijing ya 2008 alikua mwanamke wa kwanza kushinda dhahabu katika mbio zote za mita 5,000 na 10,000. Alitetea taji lake la medali ya dhahabu katika mita 10,000 kwenye michezo ya Olimpiki ya London ya 2012, na kuwa mwanamke wa kwanza kushinda mbio hizo (1000m) kwenye Olimpiki mbili mfululizo.
Dibaba alitiwa shime na familia ya wakimbiaji. Ambapo Derartu Tulu, aliyekuwa binamu binamu yake alikuwa ameshinda medali mbili za dhahabu za Olimpiki katika mita 10,000 katika michezo iliyofanyika huko Barcelona mnamo 1992 na huko Sydney mnamo 2000.. Ilionekana dhahiri kwamba wakati dada mkubwa wa Dibaba Ejegayehu aliyemzidi kwa miaka mitatu alipoanza kushiriki mbio za ushindani mnamo mwaka 1998, Ternush Dibaba angefuata dada yake muda sio mrefu. Dibaba alihamia Addis Ababa mnamo mwaka 2000 kuishi na Ejegayehu (Dada yake) na binamu mwingine ambaye pia alikuwa mkimbiaji. Alikuwa amepanga kujiandikisha shuleni lakini badala yake alijiunga na kilabu cha Jeshi la magereza. Dibaba alianza kukimbia kimataifa akiwa na umri wa miaka 15 kwenye kikosi cha vijana wa Ethiopia kwenye mbio za nyika za dunia za mwaka 2001 ambako alimaliza wa tano. Hii ilifuatiwa na ushindi wake medali ya fedha ya mbio za nyika kwa vijana yaliyofanyika mnamo mwaka 2002.
Mnamo mwaka 2003 Dibaba alishinda taji la dunia la mbio za nyika kwa vijana ambapo aliweka rekodi mbio za mita 5,000 (sekunde 14 39.94 sec), na baadaye alipata medali ya dhahabu katika mita 5,000 kwenye mashindano ya kimataifa ya Chama cha Wanariadha (IAAF) na kuwa bingwa wa dunia mdogo kabisa katika mchezo katika mbio (Mchezo wake). Ingawa katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2004 iliyofanyika huko Athenes ugiriki Dibaba alifanikiwa kuboresha muda wake wa rekodi yake ya dunia kwa vijana katika mbio za mita 5,000 hadi hadi dakika 14 na sekunde 30.88 alifanikiwa tu kupata medali ya shaba..
Baada ya kuweka rekodi ya mbio za ndani za dunia katika mita 5,000 (14 min 32.93 sec), alishinda mataji katika mbio za nyika katika umbali wa kati na umbali mrefu.. Katika mashindano na ubingwa wa dunia wa mashindano ya mbio, alikuwa mwanamke wa kwanza kushinda mbio katika umbali wa 500m na 10,000m.
Alishinda mbio za nyika za dunia za 2006 na 2008 na kuvunja rekodi ya dunia ya mita 5,000 ya mashindano ya ndani (Indoor) yaliyofanyika mwaka 2007 kwa kutumia dakika14 na sekunde 27.42, lakini katika mwaka uliofuata alilazimika kupambambana vikali ili kuweza kutetea taji lake la dunia la mita 10,000 baada ya kuwa ameanguka wakati wa mbio. Mnamo Oktoba 2008 Dibaba aliolewa na Slimhi Sihine ambaye ni mshindi mara mbili wa medali ya fedha katika michezo ya olimpiki katika mbio za umbali wa 10,000m.Majeruhi yalimfanya kusitisha kwa muda shughuli zake kuanzia 2009 hadi mwaka 2011. Miezi kadhaa baada kurudi kukimbia tena katika michezo ya Olimpiki ya London ya mwaka 2012, alishinda medali ya dhahabu katika mita 10,000 na ya shaba katika mita 5,000. Dibaba alikimbia mbio zake za kwanza za nusu marathon zilizofanyika huko Uingereza. Dibaba alishinda tena medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia ya mwaka 2013 katika mita 10,000 na mwaka 2014 alishindana katika mbio zake za kwanza za marathon. Kwenye Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro 2016, alitwaa medali ya shaba katika mbio za mita 10,000. Mwaka uliofuata alishinda mbio zake za kwanza za marathon zilizofanyika huko Chicago Marekani.
Hebu mwangalie Dibaba hapa utadhani sio mwanamke