Mjue Tony Adam au Mr Arsenal

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Anaitwa Tony alexander Adam, amezaliwa tar 10 oct 1966 katika kitongoji cha ROMFORD, ENGLAND

alianza kucheza Soka katika academy ya arsenal 1980-83 ilipofika mwaka 1983 alipandisha Timu ya wakubwa Kama beki wa kati,

Akiwa timu ya wakubwa alionesha uwezo mkubwa huku akiisaidia Arsenal kutwaa UBINGWA WA FIRST DIVISION CHAMPIONSHIP mara mbili msimu wa 1988 na msimu wa 1991.

Anatajwa katika orodha ya WACHEZAJI BORA 100 WA SOKA BORA WA MUDA WOTE,

Akiwa Arsenal alikuwa Mlevi sana, na rafiki ya Ray parlour, wote wanatokea Kitongoji cha ROMFORD

Kutokana na kukithiri kwa tabia za ulevi katika klabu ya arsenal kulisababisha Timu kufanya vibaya, huku kwa kipind hicho wakiambulia MATAJI ya league cup na UEFA WINNERS CUP mwaka 1993, hii ilipelekea mwaka 1995 kocha Graham kufukuzwa.

Mwaka 1996 alikuja mzee ARSENE WENGER ambaye aliwabadilisha mienendo ya maisha ya wachezaji wengi walevi wa Arsenal akiwepo TONY ADAM, na RAY PARLOUR, LE DIXON, NIGEL WINTERBURN aliwabadilishia life style kuanzia mazoez had Lishe,

Walibadilika walipigana kufa na kupona na mwaka huo huo walitwaa DOUBLE (FA CUP & EPL) msimu wa 1997/1998

Huku TONY ADAM akiwa captain mpiganaji, aliisaidia Arsenal kutwaa Tena double msimu wa 2001/2002.

Anafahamika kama MR. ARSENAL kutokana na mapenzi yake kwa arsenal, aliwahi kusema LETA MKATABA ATAUSAINI BILA KUUSOMA kuhusu kuchezea Arsenal

NI MMOJA KATIKA YA WATU WACHACHE WALIOTWAA EPL NA FIRST DIVISION

PIA NI MMOJA KATI YA WACHACHE WALIOTWAA MATAJI KTK MIONGO MINNE (1988, 1991,1997,2002)

Clubs: Arsenal
Honours: 2 Division One Championships,
2 Premier League Titles,
3 FA Cups,
1 European Cup-Winner’s Cup, 2 League Cups
Caps: 66, 5 goals

JE WEWE UNAMFAHAMU VIPI HUYU LEGEND WA EPL?
 
Mguu wa shingo mguu wa roho..beki kisiki kipindi hiko ilikuwa ARSENAL sio arsenal....nilishawahi kupeana mkono na huyu jamaa nikiwa na umri wa miaka6 pale HIGHBURY SFADIUM hilo ndilo ninalolikumbuka na ndio limenifanya niwe shabiki lialia wa arsenal mpaka leo hii
 
Lee Dixon, Nigel Winterburn, Martin Kewon, Steve Bould na yeye waliunda ngome imara iliyoitwa ukuta wa Berlin pale Arsenal.
kwa faida ya wengineo, huo ukuta ulioutaja ndio ulikuwa hivyo hivyo hadi timu ya Taifa ya England.

Ni kama kwa miaka ya karibuni ukuta wa Juve ulioundwa na Buffon na mabeki wake Barzagli, Bonucci na Chiellini ulikuwa unahama hivyohivyo hadi timu ya Taifa.
 
hivi tony adams hana undugu na victoria adams posh spice mke wa beckham?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…