kinjekitile70
JF-Expert Member
- Oct 11, 2017
- 1,072
- 1,424
Habari binafsi
Tufuatane hapa chini
Aliingia Kyoto mwaka 1579 mamia walikusanyika kumuona mtu wa kwanza mweusi kuingia mjini hapo. Kiongozi wa mji aliamuru aoshwe kwa kile alichoamini kuwa ile rangi nyeusi sio yake bali amejipaka. lakini YASUKE alishinda yote na kuwa Samurai mweusi wa kwanza..
Kwa wachezaji wa game la NIOH, mpiganaji mweusi anaetumia shoka anaweza asiwe mgeni kati yenu. Anaitwa Yasuke, ni mrefu, mweusi mwenye mapana na alievalia mavazi ya wapiganaji wa kijapani. Yawezekana miongoni mwetu ni mashabiki wa SAMURAI huyu anaepigana kwa kutumia shoka
lakini pia wapenzi wa filamu za Hollywood, mwaka 2017 THE LIONSGATE’S FILM walianza kutengeneza filamu zilomhusu SAMURAI mweusi tena wa Kiafrika huko mashariki ya mbaaaaali kabisa, katika nchi ya JAPAN. Nikufahamishe tu yakua, zote hizo zinayahusu maisha ya kweli ya.
Muafrika wa kwanza na mtu kwanza ambae sio m-japan kuwa SAMURAI katika nchi ya JAPAN.
Wakati bado uhalisia wa asili yake ukiwa ni sintofahamu, zipo nadharia zinazoeleza yakuwa YASUKE alikua ni mtu kutoka Mozambique, hii ni kulingana na maelezo ya mwana historia...
FRANCOIS SOLIER, Lakini baadhi ya Makala zikieleza alikua ni mtu alietokea kule Sudan Kusini na nyingine zikidai alikua ni Mhabeshi kutoka kule Ethiopia. Mbali na yote lakini uhalisia wake hadi leo hii umebaki kuwa na sintofahamu.
Miaka Zaidi ya 500 iliyopita, historia inaeleza..
kuwa, Yasuke aliingia nchini JAPAN akiwa kama msaidizi wa M-missionary alieitwa ALLESANDRO VALIGANO ambaye alikua ni msimamizi wa safari za wa-Missionary huko Afrika ya mashariki, Afrika ya kusini na Mashariki ya mbali hadi Uchina.
Rekodi za kuwa Yasuke aliingia nchini Japan kama mtumwa bado hazina ushahidi wa kutosha, wanaoziunga mkono hudai alikua ni mtumwa alietoka Afrika kama matokeo ya biashara ya utumwa. Na wengine hudai alikua ni mtumwa aliezaliwa ulaya katika nchi ya Ureno.
Mengi yamekuwa yakidhaniwa na ukweli wake bado haujapata muafaka.
Mpaka unafika mwaka 1579 Yasuke alikua katika ziara mbalimbali na M-missionary bwana Allesandro Valigano, mpaka hapo mwanzoni mwa mwaka huo alipoingia katika mji mkubwa wa Kyoto. Mji ulikuwa chini ya kiongozi..
mkubwa tena mwenye nguvu, kiongozi ambaye anakumbukwa katika historia ya nchi ya Japan katika mchango wake wa kuiunganisha nchi hiyo. Kiongozi huyu aliitwa Daimyo ODDA NABUNAGA.
Habari za mtu mweusi kuingia katika mji wa KYOTO zilikua ni kubwa.
watu wengi hawakuona mtu kama huyo zamani…mamia walikusanyika na watu wengi walikufa kutokana na mikanyagano ya kutaka kumuona Yasuke mtu wa kwanza mweusi kuingia katika mji huo. Hii ni kwa mujibu wa mwana historia Lawrence Winkler.
Hamaki na staajabu ilitawala pindi.
YASUKE alipofika mbele ya macho ya kiongozi wa Kyoto aloitwa Daimyo Odda Nabunaga, Nabunaga kwa mara ya kwanza alidhani Yasuke amepakwa rangi nyeusi, hivyo haraka aliamuru watumishi wake kumuosha tena kumsugua Yasuke ili waondoe rangi yake nyeusi ambayo yeye alidhani imepakwa.
kwa juu ya rangi asilia. Lakini punde alijiridhisha yakuwa yasuke alikua ni mtu mweusi. Akiwa ni mtu aliye staajabu mno, bwana Oda Nabunaga alipokutana na Yasuke kwa mara hiyo ya kwanza…maneno haya yalirekodiwa kutoka kinywani kwake..
“ukurasa mweusi umekuja toka katika..
nchi za wakristu, anaonekena kama ana umri wa miaka 26 au 27. Mwili wake wote una rangi nyeusi kama ile ya shoka. Mtu huyu anaonekana mwenye afya na anamuonekano mzuri. Zaidi ya hayo..nguvu zake ni Zaidi ya watu 10. Jina lake ni yasuke, ni mweusi na rangi yake ni kama mkaa
Niwazi Nabunaga alionekana kuwa shabiki wa Yasuke, inasemekana kuwa..kabla ya kuonana na nabunaga, Yasuke alishakaa kwa kipindi Fulani nchini japan na hivyo alipata wasaa wa kujifunza lugha ya kijapan mapeema kabisa. Na punde alipokutana na nabunaga.
Umahiri wake wa kuongea kijapan ulimfanya Nabunaga aweze kuvutiwa na yeye. Alizidi kushawishika na umbo lake, Rangi lakini pia nguvu zake…Daimyo Odda Nabunaga alimtoa Yasuke katika aina zote za utumwa na manyanyaso…kisha akamfanya kuwa kibaraka wake, tena msaidizi wa karibu.
Alipatiwa nyumba, pesa na akafanyiwa sherehe ndogo….na baada ya muda bwana Odda Nabunaga alimpatia heshima ya kuwa SAMURAI…na hapo Yasuke akawa mtu mweusi wa kwanza kuwa Samurai. “urefu wake ni wastani wa futi 6 na inchi 2…alikua mweusi na ngozi yake ilikua kama mkaa” haya..
aliyaeleza samurai mwenzake Matsudaira Letada katika kitabu chake mnamo mwaka 1579.
Pamoja na kusifiwa kwa vitendo vya kibaguzi, wajapani hawakuweza kabisa kumbagua kwa aina yeyote ile bwana Yasuke kwakua, Tangu mwanzo walikua na taratibu za kuabudu baadhi ya masanamu..
ya budha meusi..kwa hivyo rangi nyeusi walikua wanaitukuza na kuiheshimu.
Historia ya Yasuke nchini Japan haikudumu kwa muda mrefu, ilipofika mwaka 1582 jenerali mmoja alifanya uasi na kumlazimisha Odda Nabunaga ajiue mwenyewe kwa heshima yake kama samurai, historia inaeleza..
yakuwa Yasuke alipewa maagizo ya kutoroka pamoja na mtoto wa Oda nabunaga. lakini haukupita muda wote wawili walikamatwa…na kama samurai alikabidhiwa jambia ili ajiue mwenyewe. Lakini kwa daharau Jeneral huyu alimfukuza yasuke kama mnyama na kudai yeye sio mjapani hawezi..
kupewa jambia ajiue kwakua yeye ni kama mnyama asie jua chochote.
Na kuanzia hapo habari zake zikaishia pale, achilia mbali mchango mkubwa alioutoa katika vita chache alizopigana katika kipindi kifupi tu alichokua Kyoto mwaka 1582 ukawa mwisho wa Yasuke na huku baadhi ya nukuu.
zikieleza kuwa alirudishwa katika makanisa ya wa-missionary na alipotokomea hapakujulikana. Habari za shujaa huyu wa kiafrika zimetokea katika baadhi ya vitabu vya hadithi na historia ambavyo vyote vimekua vikiishia na mwisho mbaya wa Nabunaga kujiua na yasuke kutokomea pasipo.
Ahsante kwa usikivu
Msisahau kunywa dawa za Madagascar
Sent using Jamii Forums mobile app