Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MWINYIMBEGU DIBIBI- MZALENDO WA KIAFRIKA ALIYESAHAULIKA
Ahmed Dibibi
Si wengi wenye kulifahamu jina hili na wengine yawezekana ikawa mara ya mwanzo kulisikia.
Mwinyimbegu Dibibi kwa watu wa makamo na wazee si jina geni masikioni mwao, wenyeji wa Miji ya Upwa wa Tanganyika ya Kale na Unguja wamelisikia sana miaka hiyo.
Huyu ni alama ya uzao Mkuu wa Familia ya Dibibi Wasagala wa Kilosa na Wazaramo wa Kisarawe, kwa wale waliofika Msanga basi kuna sehemu panaitwa "MSANGA KWA DIBIBI" ni Kijiji maarufu hadi hii leo, pia ni kituo cha magari ya abiria na wengine wanapatumia kama kiliofu- anuani ya kuwafikisha huko waendako.
Mzee Didibi alikuwa miongoni mwa waasisi wa Chama cha Siasa cha TANU akiongoza harakati za kudai Uhuru katika Miji ya Dar es Salaam, Pwani na viunga vyake akiwa pia miongoni mwa wafadhili wakubwa wa Chama hicho katika Wilaya ya Kisarawe ya wakati huo.
Mchango wake ni mkubwa ambao umesalia katika shubaka ya watu wachache kwani hata katika shajara za Taasisi hatuoni wala kusikia wakielezea mchango wa mwanasiasa huyu ambaye pia alikuwa mfanyabiashara.
Jina lake lilivuma akikijenga na kueneza siasa za TANU katika Wilaya ya Kisarawe ambayo baadae imegawanywa imetoka Wilaya za Ilala, Kisarawe na baadae Mkuranga wakati huo ilikua moja (Kisarawe).
Mzee Dibibi, hakuwa peke yake katika harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika, aliungana na wanasiasa wengine, Sheikh Suleiman Takadiri, Dossa Azizi, Abdulwahid Sykes, Bi Tatu binti Mzee, John Rupia, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bibi Titi Mohamed, Rashid Mfaume Kawawa na wengineo ambao kama nitawaorodhesha hapa leo, basi naweza kujaza kurasa kwa kurasa.
Katika barza maarufu za Dar es Salaam, Mwinyimbegu Dibibi alipiga soga la siasa, mipango na mikakati na watu mashuhuri wa Dar es Salaam.
Katika Mitaa ya New Street sasa Lumumba, yalipokuwa Makao Makuu ya TANU ambayo sasa ni Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Dodoma, ilikuwa ni kawaida kumkuta Mzee Dibibi akiwa na wanasiasa wenzake wakipanga mambo kadhaa wa kadhaa. Mzee Dibibi alikuwa na makaazi yake katika Mitaa ya Kariakoo, hakuwa mshamba wa kuja, bali alikuwa mzalia kindakindaki wa Mzizima (Dar es Salaam).
Hakuna aliyetilia shaka uzalendo wake. Mwinyimbegu Dibibi hakutoa mchango tu katika siasa, bali amekuwa chachu ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mzee Dibibi lilipokuja wazo la kuwa na Chuo Kikuu katika Tanganyika, hakurudi nyuma, ni miongoni mwa watu waliotoa pesa na mchango mkubwa wa hali na mali katika kuanzisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (rejea tovuti ya Chuo Kikuu).
Si wengi wenye shauku ya kufahamu waliotoa michango kusimamisha TANU na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini kwa wale wadadisi na wenye kukumbuka wema na hisani, lazima watataka kufahamu Wazalendo kama Mzee Alhaji Mwinyi Dibibi aliyetoa kiasi cha pesa taslimu na hii ilikuwa mnamo mwaka 1958 wakati huo vuguvugu la Waafrika kutaka kuondoa ukoloni na kujitawala wenyewe lilivyopamba moto.
Ari ya Waafrika wa Tanganyika kutaka kujitawala ilikuwa imemjaa kila mtu, kike, kiume, wa Mjini na Mashamba ilmuradi watu walichoka kutawaliwa na wageni.
Hakuwa yeye tu aliyechangia kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, bali kulikuwa na Wazalendo wengine 110 waliotoa mchango wa pesa taslimu.
Mwanafalsafa mmoja, Frederick Douglass aliwahi kusema kwamba "Elimu ni Ukombozi” kwa hakika, wanamajumui hawa wa Kiafrika kutoka Tanganyika walifahamu ubora wa elimu na umuhimu wake katika kujenga jamii iliyoelimika ambayo wataitumia kama silaha na nyenzo katika kupambana na maisha yanayobadilika kila uchao huku wakikabili changamoto zinazohitokeza.
Kwa kutumia nyenzo ya elimu kama silaha ya kupambana na vikwazo vilivyowekwa na Wakoloni, Waafrika wakielimika katika elimu bora ingewasaidia kufikia malengo na ahadi zao katika kuondoa vizuizi vilivyowekwa na mfumo wa ukoloni.
Mzee Dibibi ni mmoja wa watu niliowahusudu sana kiasi cha kunishawishi na kunipa ari ya kipawa changu kutafuta elimu na taaluma ya ujuzi na kuweza kuwasaidia na wengine ambao wanahitaji maarifa na weledi wetu.
Jina lake limeorodheshwa katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akipewa nambari 96.
Alhaj Dibibi alikua mfanyabiashara mkubwa wa vyombo vya usafiri (magari) (Dibibi Trans), chakula alikua akitoa vyakula Kama mihogo na mahindi katika mashamba yake, Kigoma na Kilosa, kiasi cha magari yake yalipewa jina la 'Muhogo wa Kigoma Msanga kwa Dibibi' kiasi cha bendi ya NUTA Jazz kutunga wimbo maarufu wa Muhogo wa Kigoma Msanga kwa Dibibi na mpaka leo kijiji kipo Msanga Kisarawe Pwani kinajulikana kama Msanga kwa Dibibi kama nilivyoeleza awali.
Alhaji Didibi hakuishia katika siasa, elimu, bali alijenga misikiti hapo kijijini na madrasa żenye ubora huku akiendelea na shughuli zake za biashara ya maduka ya Jumla na Rejareja, Jijini Dar es Salaam na Pwani enzi za Tanganyika kabda ya uhuru na baada ya uhuru na baadae Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa hakika kila aliyetenda wema katika mgongo wa dunia anahitaji jazaa njema, nami nachukua fursa hii kuweka kumbukumbu hii iwe rejea kwa wale wataopenda kufanya utafiti juu ya historia ya TANU, siasa za Tanganyika kabla na baada ya Uhuru, maendeleo ya elimu Tangayika na baadae Tanzania, kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alhaj Sheikh Mwinyimbegu Dibibi Msagala alifariki mwaka 1982 akiwa na umri wa miaka 92. Amezikwa katika makaburi ya Wasagara yaliopo kijiji cha Chang,ombe A Kata ya Marumbo Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
UZARAMONI Mungu Ailaze Roho yake Mahala Pema.