Zanzibar. Mjumbe wa Bunge la Katiba kupitia Chama cha Allience for Tanzania Farmers Party (AFP), Rashid Yussuf Mchenga amevuliwa uanachama kwa madai ya kughushi saini ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Shaibu Masoud Salum. Uamuzi huo ulitangazwa juzi na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Said Soud Said.
Said alisema saini hiyo aliyotumia kumhalalisha katika ombi la barua yake iliyokwenda Ikulu ya Zanzibar, haikusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa AFP Zanzibar na tayari wamefungua kesi Kituo cha Polisi cha Madema.
Alisema majina yaliyotumwa Ikulu kwa uteuzi ni ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Rashid Mohamed Rai aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba, Mahadhi Mohamed Mahadhi, (Soud) na mkewe Farida Juma Khamis.
Naye Mchenga alisema chimbuko la kuibuliwa mgogoro huo ni mwenyekiti na mkewe kukosa kwenye uteuzi huo na kwamba, hawezi kughushi saini ya mtu.
"Ni wivu wa mwenyekiti wetu. Amechukia kutoteuliwa yeye na mkewe. Hajui riziki ni mafungu saba, Bunge hili limemtoa udenda na sasa anatapatapa tu mimi ni mjumbe halali," alisema.
source: Mwananchi gazeti