Pre GE2025 Mjumbe Halmashauri ya Kuu CCM: Vijana wa CCM wanaowatukana viongozi kwenye magroup ya Whatsap hatutawapa nafasi za uongozi

Pre GE2025 Mjumbe Halmashauri ya Kuu CCM: Vijana wa CCM wanaowatukana viongozi kwenye magroup ya Whatsap hatutawapa nafasi za uongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Mkoa wa Geita, Evarist Gerves, amekemea vikali tabia ya baadhi ya vijana wa chama hicho kuwatusi viongozi na watu wanaotangaza nia ya kugombea kwenye uchaguzi mkuu kupitia makundi ya WhatsApp.

Alisema tabia hiyo ni kinyume cha maadili ya CCM. Evarist alitoa kauli hiyo katika ziara yake ya Kata ya Lulembela, Wilaya ya Mbogwe, ambapo alieleza sababu za Mkutano Mkuu wa CCM kumtaja Rais Samia Suluhu Hassan kama mgombea wa urais.

Alisema baadhi ya viongozi wanawashirikisha vijana kwa lengo la kuwatukana wanasiasa wengine na alitoa wito kwa vijana kuzingatia maadili ya chama.



Source: EFM Tanzania
 
Back
Top Bottom