Pre GE2025 Mjumbe Kamati Kuu CCM, Mamuya: Hakuna anayeweza kushindana na Dkt. Samia

Pre GE2025 Mjumbe Kamati Kuu CCM, Mamuya: Hakuna anayeweza kushindana na Dkt. Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Halima Mamuya amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hatakuwa na mpinzani katika uchaguzi mkuu wa 2025 kwa sababu licha ya kwamba ni Rais lakini pia ni Mama mlezi wa Taifa.

Amesema kutokana na falsafa ya Rais Samia ya 4Rs nchi itabaki kuwa na Amani tofauti na nchi nyingine ambazo zimekuwa zikiingia kwenye vita

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ameyasema hayo leo Februari 19, 2025 Jijini Arusha wakati wa hafla ya Uhamasishaji wa kutoa Elimu ya Nishati safi kwa Viongozi wa Baraza la Wazee Jijini humo iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo.

Aidha katika hafla hiyo Wazee wa baraza hilo wamekubaliana kuunga mkono maamuzi ya Chama cha Mapinduzi CCM kumteua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Dkt. Hussein Mwinyi na Emmanuel Nchimbi kuwa wagombea.

 
CCM ..kama mnajiamini wekeni Tume HURU halafu ACHENI polisi wafanye majukumu Yao.... Muonge kama hata Sasa mbili asubuhi mtafika ....mapema sana
 
Back
Top Bottom