Pre GE2025 Mjumbe UVCCM Geita, Sagayika awataka Vijana kuacha kubeba mabegi ya wagombea

Pre GE2025 Mjumbe UVCCM Geita, Sagayika awataka Vijana kuacha kubeba mabegi ya wagombea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570

Hao vijana wenyewe wanaopewa ushauri huu ndiyo kwanza wako busy na uchawa​

===
Ikiwa imebaki miezi minane kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, vijana wametakiwa kuacha tabia ya upambe na kubeba mabegi ya wagombea badala yake wagombee nafasi mbalimbali.

1739793844218.png

Msingi wa hoja hiyo iliyotolewa leo Februari 17, 2025 na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Mkoa wa Geita, Reuben Sagayika ni kusaidia kupata vijana wengi katika ngazi za maamuzi ili changamoto zao zifikishwe.

"Ninyi vijana ni vizuri mkagombee, ili mnapopata nafasi ndani ya Serikali mnawapigania vijana wenzenu walio nje na kuwasemea shida na changamoto zao. Sasa mkiwa mnabeba mabegi ya wagombea na kuwa wapambe tu, nani atawasemea huku? Vijana tuamke," amesema Sagayika katika kikao cha baraza la UVCCM mkoani Geita.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom