The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa (Viti Vitatu bara) Ndg. Shamira Mshangama amepokelewa katika Wilaya ya Musoma mjini, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana wa CCM katika mikoa, Wilaya, kata, matawi na shina kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu 2025.
Ndg @shamiramshangama baada ya kufika mkoani Mara alihudhuria BARAZA la Umoja wa Vijana wa CCM katika Wilaya ya Musoma mjini Kama Mgeni Rasmi ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana katika Wilaya ya Musoma mjini na kuwaasa kuendelea kukijenga Chama kwa Uzalendo ili kuhakikisha ushindi wa kutosha kwa Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu 2025 kwa kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na madiwani wa CCM kwa kura nyingi na za kishindo zaidi
Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Alisisitiza “Vijana tuna jukumu la kutafuta kura za Samia na wagombea wengine wa CCM. Hivyo ni wajibu wetu kuweka mipango ya kutosha juu ya kuzitafuta kura za CCM”.
Sambamba na hayo Ndg. Shamira alipata wasaa wa kutembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Jumuiya ya Umoja wa vijana (katibu) inayoendelea kujengwa, pamoja na kuchangia shilingi milioni 1, alihimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri ili kukamilisha ujenzi kwa wakati.