MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
Shekhe Hamid Jongo ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Maulamaa na Imamu wa Msikiti wa Manyema, Kariakoo Dar es Salaam, amewageukia wanaokataa kura ya wazi akisema ni wanafiki na waoga, huku akiwatupia vijembe wasomi, akiwaambia, hamuoni kwa macho, hata kupapasa! aliwashangaa wanaotaka kura ya siri wakati walipodai posho waliweka mambo hadharani.
Tulitoa hoja zetu kuhusu posho kwa uwazi bila kunongona, wananchi wakatuzomea, magazeti yakaandika, sasa kura tunataka kwenda kimyakimya. Na mimi naunga mkono mpaka kieleweke. Hapana, tupige kura ya waziwazi tufahamike, hakuna hoja ya mantiki ya kujificha. Kama posho hatukunongona, tunaogopa nini? alihoji Shekhe Jongo.
Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM) amesema kama wazee wa zamani walimwogopa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika kudai Serikali ya Tanganyika, basi imekula kwao.
Hili la Tanganyika hatulitaki. Kuna watu wanadai hapa kuwa wao tu ndio jasiri, wakati ni waoga tu. Majasiri wako wengi, mimi ni jasiri na watu wanajua. Hata Mandela alikuwa jasiri sana. Kama mlishindwa kuipata Tanganyika yenu wakati huo, imekula kwenu.Kama mlimwogopa Mwalimu hadi akafa ndio mnadai Tanganyika, imekula kwenu. Tuko Mwalimu mwingine, alisema Lusinde akishangiliwa na wajumbe wenzake. Watu wanateseka kwa foleni pale kumsubiri Mzee Pinda na viongozi wengine wapite, leo mnataka kuwa na viongozi sita. Acheni uroho wa madaraka.
Lusinde aliyekuwa akizungumza huku akitoa mifano mbalimbali yenye kufurahisha, alionekana dhahiri kumjibu Mjumbe mwenzake, Christopher Mtikila aliyedai ndiye jasiri pekee nchini na anayejulikana kuwa ni muumini wa Tanganyika.
Kwa upande wake, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano, Job Ndugai alionya matumizi mabaya ya lugha hasa kuhusu masuala ya Muungano.
Tumevumilia sana, mahali penyewe pa kuongea ndio hapa. Lakini tuwe makini, vinginevyo tutagawana mbao hapa. Tumekuja wamoja, tuondoke wamoja. Tukianza lugha za ajabu ajabu hapa, hatutafika, alisema Ndugai. Kauli ya Ndugai ilitokana na Mjumbe Said Ali Mbarouk aliyesema kuwa utungaji wa Kanuni ni lazima uanze kwa kuipa Zanzibar maamuzi yake, kwani kwa miaka 50, kumekuwa na uonevu na dhuluma kubwa.
Chanzo: Habari leo.