Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Marium Mamuya: Ushindi wa serikali za mitaa CCM tumeutolea jasho

Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Marium Mamuya: Ushindi wa serikali za mitaa CCM tumeutolea jasho

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa CCM na mlezi wa chama hicho mkoa wa Njombe, Marium Mamuya amesema ushindi mkubwa walioupata wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 haukuwa rahisi na unaashiria ugumu utakaopatikana kwenye Uchaguzi Mkuu hapo mwakani.

Ameeleza hayo mkoani Njombe alipokuwa akizungumza na wajumbe kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa uliofanyika leo mkoani humo.

"Ninawapongeza sana kwa kazi kubwa mliyoifanya kwa sababu ushindi tulioupata hatukupata bure, kila mmoja ametoka jasho kwa namna yake na hili jasho tulilotoka linaashiria huko mbele tutoka jasho zaidi au tutapunguza kwa sababu tutakuwa tumejiandaa vya kutosha," amesema Mamuya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe ambaye ni mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga (Jah People) amewaonya viongozi wa Chama hicho wanaogeuka na kuwa mawakala wa wagombea jambo ambalo linatajwa kupelekea kukigawa chama.

"Viongozi wenzangu tusimamie utaratibu wa chama unavyotaka, mtu yeyote tutakayemkuta anakwenda nje ya kanuni msishangae kuona anaitwa kwenye vikao vya maadili kwa sababu kwenye maeneo yenu wapo watu wanafanya makusudi kama chama hakipo, acheni kwa sababu muda ukifika chama kimeweka utaratibu mzuri," amesisitiza Sanga.

Screenshot 2024-12-20 180539.png
 
Back
Top Bottom