OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Simulizi ya MK14 Meddie Kagere
“Mimi si muongeaji, naamini kila kitu kina sababu na hakiwezi kuwa na mwisho, katika soka kocha ni mtu ambaye anaweza kumfanya mchezaji kuwa kwenye ubora wa hali ya juu, lakini pia huyo huyo akakuporomosha kiwango".
“Nakumbuka kuna kipindi kocha anakuonyesha dhahiri hakutaki, au anakuchukia sababu tu wewe mchezaji ni staa"
“Sven aliniambia kwenye timu yake hapendi mastaa, nilimwambia hiki kinachotokea sio mimi nataka ila ni mashabiki ndiyo wanafanya hivyo sababu wanaridhishwa na kazi yangu,”
“Watu walikuwa wakiniona, nikipewa nafasi hata kama ni dakika 10, naenda kufanya kazi, kwani niliamini sichezi kwa sababu ya kocha apate matokeo, la hasha bali nikifanya vizuri ndipo natengeneza jina langu zaidi, hivyo nikipewa nafasi hata kama ni dakika mbili nitapambana kadri ya uwezo wangu,”.
Anasema bifu lake na Sven lilianzia kwenye timu ya taifa ya Rwanda, ambako aliomba kazi.
“Shirikisho waliniuliza kuhusu yeye, niliwaambia ni kocha mzuri, anajua kufundisha lakini ana changamoto zake, akisema ni hivi basi ni hivyo hivyo hata kama anakosea.
“Niliwaeleza ukweli wa jinsi alivyo Simba, anabishana na kila mtu ila wakimuweza kwenye tabia zake basi ni kocha mzuri, alifahamu hilo na akaja kuniambia kwamba nimemchongea, kuanzia pale tukawa tupo tofauti.”
Anasema alipokuja Gomes, yeye Kagere alikuwa akifahamiana nae kabla kwani aliwahi kumfundisha Rwanda.
“Pia naye aliwahi kuomba kazi Shirikisho, aliniambia nimuunganishie kwa kuwa kwa kiasi fulani wananisikiliza na yeye Gomes anafahamu hilo.
“Nilipowaeleza wakaniuliza kwanini ananiweka benchi, nikawaambia pia amefuata mfumo wa Sven, kwani alikuta nawekwa benchi na yeye akapita humo humo, nilikuwa na mabao 11, nikawa benchi hadi Bocco na Mugalu wakanipita"
My Take
Kuna wakati huwa naelewa kwa nini uongozi huingilia mipango ya kocha. Kuna makocha ni majuha