Botolani
Member
- Jul 23, 2022
- 6
- 8
Miongoni mwa mada muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu ni Nishati ya kupikia. Historia inasomeka kuwa mwanadamu alianza kupata maendeleo makubwa (evulution) baada ya kujua namna ya kudhibiti moto na kuutumia kupikia na kisha kwenye shughuli nyingine. Alipoanza kupika, ndipo mabadiliko makubwa ya kimwili na kiakili yalianza kutokea taratibu mpaka kukatokea ustaarabu ambao umekuwa ukiendelea na mpaka leo hii. Hivyo, nishati ya kupikia imechangia pakubwa sana kutufikisha hapa na kuwa hivi tulivyo.
Suala la chanzo gani cha nishati ya kupikia sasa ndio limekuwa jambo linalojadiliwa sana. Mabadiliko ya tabia ya nchi na uharibifu mkubwa wa kimazingira umeibua hoja,mikakati,maoni,mapendekezo na hatua nyingi za kutaka kukomesha matumizi ya mkaa na kuni kama chanzo cha nishati ya kupikia,licha ya kuwa vyanzo hivi vilishatumika kwa muda mrefu kiasi cha watumiaji wake kuwa na muunganiko wa kihisia (emotional relationship) na vyanzo hivyo hasa katika nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania.
Leo matumizi ya kuni na mkaa ni mojawapo ya vitu vinavyotajwa kuwa si salama kwa mazingira na afya na tayari harakati za kuuzuia zimekuwa zikifanyika hapa nchini. Hatahivyo,harakati hizo zinapata wakati mgumu kutokana na ukweli kwamba hali ya maisha ya watanzania inawaaminisha kuwa vyanzo hivyo ndio hasa vinavyowafaa kutokana kwanza na unafuu wa bei,pili upatikanaji kwa urahisi na katika vipimo ambavyo wanavihitaji kwa wakati husika na kuvimudu.
Hatahivyo, mnamo mwaka 2019 aliyekuwa waziri wa masuala ya mazingira nchini, Ndugu January Makamba katiaka moja ya hotuba zake aliweka wazi namana ambavyo matumizi ya mkaa yanavyoathiri na kutishia mustakabali wa taifa kimazingira pamoja na afya za raia wake. Tafiti zinaonyesha kuwa kwa kila dakika moja, kiasi cha misitu yenye ukubwa sawa na kiwanja cha mpira hukatwa kwaajili ya mkaa! Kwa upande mwingine, tafiti zinasema kuwa moshi unaopatikana kutokana na matumizi ya mkaa athari zake huua watu 22,000 kwa mwaka. Idadi hii ni sawa na vifo takriban 60 kwa siku, inatisha! Pia gharama za kiafya zinazotokana na matumizi ya mkaa ni takribani dola bilioni mbili kwa mwaka.
Matokeo kuhusu athari za matumizi ya mkaa kiafya na kimazingira kwa sasa yanafahamika zaidi ya ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, lakini bado matumizi yake yapo palepale. Hivi karibuni kwa jiji la Dar pekeyake imeonekana kuwa mkaa unatumika kwa kiwango cha 88% ya shughuli zote za mapishi.
Na ikumbukwe kuwa kila baada ya miaka 12 idadi ya watu jiji Dar inaongezeka mara mbili (double), na kila ongezeko la 1% linapelekea ongezeko la matumizi ya mkaa kwa 14%, kwa mujibu wa Benki ya dunia. Kwahiyo ndio kusema kuwa mkaa unaendelea kuchanjambuga. Inaweza isiwe wazi sana lakini ukweli ni kwamba, nyuma ya bishara hii ya mkaa kuna vibopa ambao wanatengeneza mabilioni ya pesa kupitia biashara hii. Sheria ya misitu inakataza ukataji wa miti ya asili bila kibali maalumu ma hairuhisiwi kabisa kuvuna miti katika maeneo ambayo yametengwa na kuwekewa mpango maalumu wa usimamizi, lakini ndani ya jiji la Dar tu zaidi ya tani 2000 za mkaa huingizwa kwa siku!
Haya ni takriban magunia 40,000 ambayo kwa bei ya wastani yakiuzwa kwa shilingi 50,000 kilamoja ni sawa na shilingi za kitanzania bilioni mbili na kitu! Hapo ikumbukwe kuwa karibu 70% ya mkaa huo unapatikana kimagendo. Tafiti za karibuni zinataja kuwa mnyororo wa thamani wa biashara ya mkaa nchini ni zaidi ya dola za kimarekani bilioni moja ambazo ni shilingi 2,327,000,000,000 (Trilioni mbili na bilioni miatatu ishirini na saba)! Pesa hii tufanye nusu inaingia serikalini, nusu mifukoni mwa watu.
Ama kwa hakika mkaa ni "Dhahabu nyeusi", ni tembo mkubwa katikati ya uchumi ambaye anatumia fedha zetu kutupatia fedha na kutuangamiza kwa kupitia mlango wa nyuma! Wakati "mimi na wewe" tukiubatiza mkaa sifa ya unafuu wa bei na kuendelea kuuchukulia kama bidhaa ya kimasikini iliyoundwa na masikini kwaajili ya masikini, kumbe huko upande wa pili ni sinema ya tofauti kabisa.
Hata serikali japo inadhulumiwa, lakini inapata fedha nyingi sana kupitia biashara ya mkaa. Kutokana na kasi ya ukuaji wa miji na ongezeko la watu unaopelekea pia ongezeko la matumizi ya mkaa, inakadiriwa kuwa baada ya miaka 30 ijayo nchi itakuwa katika hali mbaya sana ya kimazingira. Hiyo ndio inaipelekea serikali, pamoja na kuingiza fedha nyingi, itake watu kuhama na kuanza kutumia vyanzo mbadala vya nishati ya kipikia ikiwemo gesi(LPG) na umeme. Lakini ugumu mkubwa wa hatua hiyo ya mabadiliko ni kwamba "mkaa ni bidhaa ya rahisi" na watu wengi hawamudu gharama za kutumia umeme na gesi kupikia.
Nini kifanyike?
Sababu kubwa ya kuendelea kwa matumizi ya mkaa ni kuhusu uchumi. Watumiaji wanadai kuwa kwa hali ya uchumi waliyonayo mkaa ndio wanaweza kuumudu, na wafanyabiashara wa mkaa nao wanapata fedha nyingi kwenye bishara yao kama faida kuliko gharama wanazotumia hivyo hawakotayari kuacha. Sasa mambo mawili makubwa yanatakiwa kufanyika;
1. Kuupa mkaa hadhi yake kisera. Sera ya nishati inaainisha kuwa nishati itakayokuwa sokoni inabidi bei yake iakisi gharama za uzalishaji. Miaka yoote hii ya matumizi ya mkaa,mkaa haujawahi kuhusika ma kipengele hichi. Sasa ni wakati wa kuupa hadhi ili nao uishi sokoni kwa mujibu wa sera. Nikwambie kitu; endapo mkaa bei yake itaakisi gharama basi hakuna mahli mkaa utauzwa shilingi 2000.
Marazote kinachopigiwa mahesabu kwenye biashara ya mkaa ni vibarua na labda usafirishaji tu, lakini miti inayotumika ambayo ndio malighafi kuu haipigiwi hesabu. Na idadi ya miti inayotumika kuzalisha tani moja tu ya mkaa gaharama yake ni kubwa kuliko mkaa wote unaozalishwa. Piga hesabu ya gharama ya miti hiyo kutokuwepo kwenye mazingira,halafu piga hesabu ya gharama za miti hiyo kama ingetumika kwenye shughuli nyingine,halafu piga hesabu ya muda ambao miti hiyo imekua kuanzia ikiwa michanga mpaka kukomaa na kuwa gogo kubwa.
2. Kupunguza au kuondoa kodi zilizopo kwenye bidhaa ya gesi(LPG). Tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa wananchi wengi huona gesi kuwa ni gharama sana kwa kichukulia zile gharama za mwanzo ambazo anatakiwa kulipia kwaajili ya kupata mtungi na viunganishi kwa maramoja. Hatua ya kuzipunguzia kodi bidhaa hizi zinaweza kufanya gharama hizo kuwa nafuu na wananchi wakaweza kumudu.
Utajiri wa nchi unaotokana na maliasili upo hatarini na hiyo ni mbaya kiuchumi kwa nchi yetu ambayo asilimia kubwa ya pato lake linategemea shughuli zinazohusisha maliasili.

Upvote
2