Tetesi: Mkakati mzito wapangwa na watuhumiwa wakuu wa Escrow

Tetesi: Mkakati mzito wapangwa na watuhumiwa wakuu wa Escrow

jembe2015

Senior Member
Joined
Sep 21, 2014
Posts
118
Reaction score
71
Wakuu,habari

Taarifa za uhakika kutoka jikoni,ni kwamba hali si shwari kabisa hasa kwa watuhumiwa upande wa pili yaani ile bank ambayo kila mtu kuanzia kamati ya bunge iliogopa kutaja orodha yao pamoja na mamlaka makubwa ya kuhoji chochote na popote waliyo kua nayo.

Ni hivi ,mkakati mpya ulio pangwa sasa ni kuendelea kuwaadaa wa tz kupitia vyombo vya habari vyote,yaani Tv,magazeti(wahariri),mitandao ya kijamii na makundi ya kijamii yenye ushawishi na wanasiasa wakubwa pia wenye ushawishi.Mkakati huo ni kuendelea kuwapotosha kwa kuendelea kupiga kelele kubwa kwa watuhumiwa wa upande mmoja (mkombozi bank) ,wao ndio waonekane wanaostahili kupelekwa mahakamani,wao ndio watuhumiwa wakuu na kila kitu,ili jamii ione haki imetendeka na kusahau kabisa kuhoji kuhusu upande wa pili (stanbic bank).

Mpaka hivi navyo leta taarifa mkakati ni mzito ,pesa imeandaliwa ya kutosha,kumbukeni upande ule wa pili (stanbic bank) sio watu wa mchezo,wamejiandaa vya kutosha kifedha na wanatumia haswa kununua makundi ya watu mbalimbali,bungeni ,vyuoni,taasisi mbali mbali ili wapige kelele sana kuhusu hawa watuhumiwa wa mkombozi bank pekee,mtakumbuka kuwa hata zitto kelele zote hajawahi kuhoji juu ya watu hao wa stanbic wala kuomba orodha..

Mkakati huu ni unalenga pia kumpotosha rais juu ya suala hili.

Wakuu mtandao ni mkubwa sana,unatisha,na kama nilivyo sema hawa watu sio wa mchezo ,wanataka kutumia pesa kufanya kama yaliyo fanywa na maharamia ya madawa ya kulevya huko magerezani kiasi cha kuishi kifahari magerezani,kuonesha jeuri ya kila haina na kuwahonga hadi wakuu wa magereza.Mkakati huo pia umepangwa na wahuskia hawa (stanbic bank mgao),na wameanza kucheza na baadhi ya taasisi hasa wahariri,Takukuru wenyewe na wanafunzi vyuoni kutoa matamko,baadae mtasikia na wengine wanakuja wapo wanajipanga (wanapikwa),ila kama nilivyo sema lengo ni kutaka kuficha ukweli husijulikane.

OMBI:Mhe.rais ,tunakupongeza sana sisi watanzania na tuko nyuma yako ktk hili na mambo mengine mengi,tunaomba husikubali kupotoshwa ktk swala hili,tunaomba haki itendeke,kama unavyo eleweka kuwa wewe ni mtu wa haki ukweli na uwazi,ukasimame kusimamia ukweli na haki ktk hili na walio husika kihalali wachukuliwe hatua stahiki.Pia tunaomba uiangalie kwa ukaribu na umakini taasisi ya TAKUKURU na nyinginezo kama mahakama zinazo husika ili yaliyo tokea kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya huko gerezani yasijirudie kwenye taasisi za uma.

Nawasilisha
 
kwa akili yangu ndogo tu.. nahisi kina zitto walitudanganya kuhusu stanbic.. why wawataje wote wa mkombozi na statement juu ila wasiwataje wa stanbic???
 
Kwani JPM hajui wahusika ni wale walikuwa wamekodi IKULU 2010-2015?Au hajui kama Pesa ilitumika kwenye UCHAGUZI wa CCM 2015??

Kama unadhani hajui basi unayejidanganya ni wewe peke yako.Sisi tuliishajua Kesi itaishia pale ilipoanzia.

Amesema kwa herufi kubwa waacheni wapumzike.Sasa hao waliokuibia wanaambiwa wapumzike wewe bado unafikiri kuna kesi ya ESCROW,pole sana,watanzania wa kidigitally hatudanganyiki kipuuzi
 
kwa akili yangu ndogo tu.. nahisi kina zitto walitudanganya kuhusu stanbic.. why wawataje wote wa mkombozi na statement juu ila wasiwataje wa stanbic???

Kama saiv tu ukitaja jina mojawapo gazeti linafungiwa, je wakati ule ambapo jina hilo lilikuwa kwenye kiti cha enzi?!!!!!
 
Lazima na wale waliochukua pesa stabic bank na watajwe na wakamatwe wapelekwe kwenye vyombo vya sheria bila ya hivyo sitaunga mkono serikali ya ccm hata kama nitabaki pekeyangu
 
Pia hakuna jambo baya kama kudhani kitu na kiwaambia watu eti nitetesi au mkakati
 
Nawewe kwa kujifanya mjuaji wakati ni bonge la kilaza, matusi kama haya walitukanwa watu wakaitwa tumbili lakini baadaye tukaanza kuijua vizuri Escrow. Ujue watu tunatofautiana sana kuna watu wana data lakini hawajui kuzi-present, kumbuka wapiga kelele kama hawa wamekua wakisaidia sana kufichua maovu yaliyo chini ya kapeti, japo huwa hawayafikishi kwa jamii kitaalamu.
Msamehe tu mkuu ...hao ndo mapimbi wa pale Lumumba
 
"PESA HIZI SIO ZA KWETU NI ZAO, SISI TULIZIWEKA KWA MINAJILI YAO SASA KELELE ZA NINI?" mpaka pale hii kauri itakapopatiwa ufafanuzi ndipo nitaunga mkono nje ya hapo hii vita ni propaganda tu ya kugain popularity
 
kwa akili yangu ndogo tu.. nahisi kina zitto walitudanganya kuhusu stanbic.. why wawataje wote wa mkombozi na statement juu ila wasiwataje wa stanbic???

Kama ulifuatilia kwa karibu hoja za kina Zito wakiivalia njuga Mkombozi Bank licha ya kuweka wazi miamala yote iliyofanyika, na ukimya wao kuhusu Stanbic Bank utagundua kulikuwa na kitu cha ziada nyuma ya pazia! Licha ya kutokutajwa kwa wanufaika wa Stanbic, kulikuwa na wenye nguvu waliokusudia ile issue iwe kifo cha Mkombozi Bank! Hakuna swala la u-Dini hapa, ni pure business interests! Wenye kujua waliliona hilo vizuri sana!
 
Mbona zito anatajwatajwa sana! Mbona kuna Kafulila, Filikunjombe, Msomi Lisu, na yule aliesema hakuna profesa muwongo kama Muhongo. Au huu Uzi nao ni MKAKATI wa kulivua kanisa na UCHAFU huu mupeleke Kwa wenzetu wa baraghashia? Kama ndivyo basi kuna mengi hapo RC
 
Mleta mada kama kweli wewe ni mzalendo wataje tu humu kama noma wacha iwe noma, tunataka kuona kila aliyeshiriki kutuibia awajibishwe, hata kama ana kinga basi iondolewe, kwani kinga ni kwa ajili ya kumlinda anapofanya kazi kama kiongozi lakini kama ametuhujumu basi alimwe tu kwani hatukumtuma kutuhujumu.
 
Nadhani kama watafanikiwa kumuhonga JPM, then wana chances kubwa za kubakia salama. Otherwise hali ni tete sana.
 
Back
Top Bottom