Mkakati wa Kuingiza Nchi Kwenye Machafuko

 

Attachments

  • VID-20250502-WA0029.mp4
    13 MB
Nyie wapuuzi wachache mnaoishi kwa keki ya taifa ndio mnahisi kwa mashaka usitufundishe ujinga kulinda keki unayofaidi
 
Jambo hili sio jepesi kulisema lakini hakuna budi lisemwe bila kupindisha maneno. Viongozi wa CHADEMA wanataka vurugu na machafuko yaliyotokea Kenya na maeneo mengine duniani yatokee nchini kwetu kama njia ya kuzuia au kuvuruga uchaguzi.
Mada nzima umeiua mwenyewe kwenye mistari hii miwili, hata kabla ya kueleza hayo mengine uliyoeleza huko chini, na ambayo bado sijayasoma na sioni sababu ya kuendelea kuyasoma.

Lakini kama bado utakuwa na akili timamu, basi tueleze kwa nini serikali na CCM wasizuie hayo unayoyaita machafuko kwa kufanya jambo rahisi tu: waanze mchakato wa kufanya marekebisho wa mfumo wa uchaguzi ili wananchi waweze kuwachagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru na HAKI. Wewe tueleze hili linao ugumu gani kulifanya ili hao wanaopenda vurugu wakose hoja.

Sijui kama nilisha soma andiko lolote toka kwako humu ndani (JF), lakini kama fikra zako ni za aina hii, sina la kujutia kutowahi kukusoma.
 
Niingize na mimi kwenye pay roll niwaseme CDM
Huyu kaingzwa kwenye 'payroll' juzi juzi tu,. Sijui kama kaingia kuchukua nafasi ya Tlaatlaah', maana sijamwona humu siku hizi za karibuni.
Bila shaka alikuwa kwenye mipango ya kumwondosha Fr Dr Kitima. Naona bado anasubiri kupoe kidogo.
 
Kama mko sahihi hakuna haja ya kuwa na hofu.
Maana hao waumini wanaufahamu ukweli kuliko hao akina LEMA.

Sasa km ni kinyume chake basi kuna haja ya kurekebisha penye dosari.
 
Samahani ndugu muandishi,hivi hao waumini wakisusia uchaguzi machafuko yanatokeaje?
 
Ninachojua mimi, sio Kanisa lolote lile nchini kwa ujinga au kwa kujivuna, au chama chochote cha siasa au mwanaharakati yeyote aliyepo ndani au nje ya nchi anaweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi yetu! HAKUNA!!!!!!!
 
Kususia uchaguzi ni kuleta machafuko ama ni kupisha wenye nguvu watawale?

Mtu anaposusia kula chakula ulichomwandalia kwa hila anakuwa katenda kosa?

Serikali inayoteka na kupoteza watu, wao aah nduhu shida, hawawezi kuchochea chuki za kuleta machafuko nchini?

Mrorongo uliowekwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi wa kufuata haki za kisheria, kwanini upuuzwe na kukanyagwa na Serikali?

Acha kupotosha umma kwa mambo ya kusadikika.

Umeanzisha uzi kupotosha wapumbaf, lakini werevu huwezi waokota na uchawa wako.
 

Hahaha..mkuu hujapiga kinywaji kweli..!?
 
Kafara ni muhimu , Hasa kafara ya damu ya mtu ni ishara ya kuukaribia utajiri, ukombazi wa Taifa umekaribia soon tutakuwa kama Ulaya,
Nchi zote duniani zilizopiga hatua zilishatoa kafara,
 
Garbage, ukweli unaujua ila unaandika uongo uliojaa unafiki..... Haki haki haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…