Fahami Matsawili
Senior Member
- Mar 8, 2018
- 172
- 153
Mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita kuifungua mikoa ya Pembezoni Kiuchumi.
Mikoa ya pembezoni ina geography nzuri ya kibiashara, fursa nzuri ya kuvutia uwekezaji hasa hasa Kwa Viwanda vya Kilimo (agricultural industry) Kwa sababu Wananchi wa Maeneo haya wanafanya manunuzi ya bidhaa muhimu na huduma katika nchi jirani na vipato vya Wananchi wa mikoa ya pembezoni ni vya chini.
Uwekezaji wa Viwanda vya Nguo, Mafuta ya kula, Viwanda vya Ngano, Vyakula na Vinywaji vinaweza kufanya vizuri zaidi Kwa sababu upatikanaji wa malighafi Upo wa Mazao ya Kilimo.
Tumetumia njia ya kutangaza fursa za mikoa yetu ya pembezoni kupitia (regionals investment guide) kama haileti matokeo ya haraka ya kuwaleta wawekezaji basi Serikali inaweza kuintervenes.
Serikali kupitia Halmashauri ianzishe Kilimo cha mikataba na Wananchi (block farming system) Kwa mazao ya kimkakati alafu Halmashauri moja moja au joint venture ya Halmashauri mbili, zinaweza kufungua Viwanda vya Kilimo Kwa kununua Mazao hayo.
Mfano Viwanda vidogo vya kukamua Mafuta ya Alzeti, michikichi, Ngano, dawa, Juisi ya matunda ya Embe, nanasi, Maziwa, Nyama, n.k
Tukitegemea njia pekee ya kusubilia wawekezaji kutoka ulaya tutachelewa kufika Kwa wakati kama Taifa kwenye Safari yetu ya Maendeleo, ni muhimu twende na zote kuvutia uwekezaji na Serikali Kuintervener kwenye project za kimkakati Kwa kuwezesha Wananchi Wetu wenyewe.
Katika maeneo mengi ya mikoa ya mipakani kuna uhitaji mkubwa wa huduma za Afya siyo Kwa Wananchi wa Tanzania tu bali Kwa Wananchi kutoka nchi zote jirani kwenye mikoa ya pembezoni.
Wagonjwa kutoka nje wanakuja nchini na Taifa likaongeza Pato kama utalii wa kimatibabu (medical tourism) ambapo watu kutoka mataifa mengine husafiri kwenda nchi maalum kwa sababu za matibabu, Sekta ya Afya siyo Kwa ajili ya Wananchi tu bali ni kitega Uchumi kama Sekta ya huduma.
Ziara ya Mhe Rais Juzi mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma, tumeona akifungua Chuo cha Veta Kwa ajili ya kuandaa rasilimali watu hasa vijana, kule kigoma Umeme wa kutumia majeneretor umezimwa hizi ni jitihada za kuizisaidia mikoa hizi za pembezoni kukua Kiuchumi.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua mashine ya uchunguzi (CT Scan) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni, Kigoma.
Hospital nzuri zenye vifaa katika mikoa ya pembezoni utavutia watalii wa Afya Serikali itaingiza mapato kupitia huduma ya Afya na mzunguko wa pesa utaongezeka maeneo hayo na kuchochea shughuli za Kiuchumi kama usafiri, chakula na malazi kuchangamka.