Mkakati wa TFF kuibeba Simba dakika za majeruhi tumeushtukia

Mkakati wa TFF kuibeba Simba dakika za majeruhi tumeushtukia

libeva

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
4,465
Reaction score
3,615
1. Kupewa kadi nyekundu kwa kocha Nasri Nabi kwa kulalamika mchezaji wake kukanyagwa na Kelvin Yondani mwamuzi sijui anajua kifaransa au kiarabu? Ndizo lugha anazo tumia Nabi alizotumia kulalamika tukio la mchezaji wake kukanyagwa je swali la kujiuliza mwamuzi aliyetoa huku ni mbobezi wa lugha za mtuhumiwa? Je TFF wamemhukumuje kocha Nabi? Kwa kufuata ripoti ya kamisaa? Je kamisaa wa mchezo anauelewa wa lugha za matusi za mtuhumiwa alizotuhimiwa mpaka hukumu ikatoka?

2. Kuvutwa kwa mechi ya Yanga na Namungo ichezwe tarehe 23/04/2022 badala ya tarehe 08/05/2022 baada ya Namungo kucheza na Simba na Namungo kuna wachezaji wa Yanga watapigwa kadi aidha za njano au nyekundu ili waukose mchezo wa tarehe 30/04/2022.

3. Kwa mazingira hayo TFF wanajambo lao Yanga wakiingia kwenye mtego wa TFF majibu watayaona tarehe 30 ambako kuna mechi hiyo. Ukimsikiliza Julio kocha msaidizi wa Namungo kuna kitu wao wamekipanga ngoja tuone matokeo yahukumiwe kwa vitendo uwanjani naamini kwa bandiko hili sitegemei makosa ya mchongo au adhabu za michongo kuibeba timu fulani tusubiri.
 
Kama jinsi ambavyo Simba Sc ilibebwa kwenye Azam Shirikisho, kuitoa Geita Gold sio?
 
Uhuru umezidi sana ktk nchi hii,hivi mtu km huyu anaachwaje hivi na uharo wote huu alioutoa??.
 
Nabi anazungumza kifaransa je kwa akil yako unaona kifaransa ni lugha ya ajabu Sana had isieleweke na watanzania?

Umepita mashuleni huko madogo wanafundishwa kifaransa km kiswahili tu ,

Kifaransa now days kwa tz ni lugha ya kawaida Sana tuna madogo kitaa wanakipiga balaa ,Sasa kwa hoja yako wale wamuuz unazijua cv zao za elimu walizonazo?

Ushauri acha kukalili kifaransa ni lugha nyepes Sana na ni lugha ya kawaida muda hata mm naielewa kidogo japo sijaisoma darasan.
 
Kitete cha kutwaa ubingwa mlioupoteza kwa miaka mi 4 mfululizo sio kidogo aisee
 
Utopolo katika ubora wake kwa nini hujafikiria hii mechi imechezwa mapema ili kumpa nafasi kocha wa yanga awepo tar 30 kwa watani wa jadi yanga mnafanya umafia halafu mnakimbia kwenye media kulalamika zile milion 10 mlikuwa mnaahidi team ikiifunga simba mbona huziongelei na mtibwa wanawadai mufanye muwalipe japo kwa sasa mmewaziba mdomo.
 
Utopolo katika ubora wake kwa nini hujafikiria hii mechi imechezwa mapema ili kumpa nafasi kocha wa yanga awepo tar 30 kwa watani wa jadi yanga mnafanya umafia halafu mnakimbia kwenye media kulalamika zile milion 10 mlikuwa mnaahidi team ikiifunga simba mbona huziongelei na mtibwa wanawadai mufanye muwalipe japo kwa sasa mmewaziba mdomo.
Kwani Mtibwa walimfunga Simba au umepitiwa tu?
 
Back
Top Bottom