Sisi watumiaji wa barabara ya kutoka Njelela kupitia Miva na Uwemba Wilayani Ludewa Mkoani Njombe tunasikitika kutelekezwa kwa vifusi vilivyomwagwa kwenye barabara hiyo.
Tunaelewa lengo zuri za Serikali kuweka vifusi hivyo lakini ni mwezi sasa tangu vifusi hivyo vimwagwe jambo linalosababisha barabara hiyo kupitika kwa taabu.
Jana Desemba 4, 2024, tukiwa tunatoka Njombe kwenda Kijiji cha Njelela kupitia Miva ilibidi abiria tushuke kwenye gari na kuanza kusambaza vifusi, hivyo ili tuweze kuendelea na safari. Hii ni kwasababu magari yanakwama kwa kuwa njia ni ndogo sababu ya vifusi hivyo.
Msimu huu wa mvua barabara za huku kwetu zinatutesa sana sasa na hivi vifusi vilivyotelekezwa hapa ndo vinazidisha mateso. Tunaomba serikali izingatie umuhimu wa matumizi ya barabara hii na kukamilisha matengenezo hayo kwa haraka.