Mkandarasi Badr East Africa arejesha Sh. bilioni 27 alizoghushi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1626160205282.png

Aliyekuwa Mkandarasi wa Mradi mkubwa wa Maji wa Mwanga, Same na Korogwe, Badr East Africa Enterprises Ltd, ameridhia kurejesha fedha za mradi huo zaidi ya Sh bilioni 27 alizodaiwa kughushi na kujipatia isivyo halali.

Mradi huo ambao inatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya laki nne, alighushi nyaraka hizo na kulipwa malipo ya awali na serikali kinyume na taratibu.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya maji, Mhandisi Antony Sanga, wakati Akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo baada ya serikali kusitisha mkataba na mkandarasi huyo.

Akizungumza mbele ya viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Waziri wa Maji, Jumaa Awesu, Mhandisi Sanga alisema Mkandarasi huyo alijipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu.

Alisema mkataba wake ulisimamishwa ili kuchukua hatua ya fedha hizo kurejeshwa na kuendelea na mradi kwa kupata mkandarasi mwingine.

“Mkandarasi aliyekuwepo alituletea nyaraka feki zilizoghushiwa na kulipwa pesa kiasi cha Sh bilioni 27 ikiwa ni malipo ya awali jitihada za kuzirudisha tulizifanya na tunefanikiwa.

“Kazi iliyokuwepo baada yakusimamisha mradi na kukabidhi mkandarasi huyo kwenye vyombo vya dola alikiri kughushi nyaraka na kujipatia fedha hizo mpaka sasa yupo ndani na sheria unaendelea kufuatwa,” alisema.

Alisema wafadhili waliokuwa wakifadhili mradi huo waligoma kuendelea kutoa fedha za kuendelea na ujenzi kwa masharti ya fedha za awali zilizolipwa kwa wakandarasi zirejeshwe ili waweze kuendelea jambo ambalo serikali ipo tayari na italipa bilioni mbili.

Akizungumza na viongozi hao,Waziri Aweso, alisema mkandarasi huyo amekubali kurejesha kiasi hicho cha fedha ambapo utekelezaji wa mradi ambapo aliwatakana wataalamu wa maji kuacha tabia ya kuongeza gharama kwenye miradi kwa maslai binafsi.

“Kwa sasa fedha zinarudishwa lakini nawaomba wataalamu muache tabia ya kuongeza gharama kwenye miradi ya maji fedha hizi ni za wananchi hatuwatendei haki lakini pia miradi ya maji sio ya wizara viongozi wote mnahaki ya kuitembelea maana nataka uwazi,” alisema Aweso.

Mtanzania
 
Wahalifu wakubainika siku hizi hamuwapeleki tena mahakamani ila mnawarusha mitandaoni na kwenye vyombo vya kabari kisha soo linakuwa limeisha.

Huu ni udhaifu, inaonekana hiyo kamounu ina mahusiano na watu waziro ndani ya Chama cha Mafisadi ambacho pia ndio chanzo cha Matatizo yote nchini.
 
Tuwekee picha ikimuonyesha anarudisha hizo hela tafadhali. Tukuamini vipi sasa?
 
Aliyekuwa Mkandarasi wa Mradi mkubwa wa Maji wa Mwanga, Same na Korogwe, Badr East Africa Enterprises Ltd, ameridhia kurejesha fedha za mradi huo zaidi ya Sh bilioni 27 alizodaiwa kughushi na kujipatia isivyo halali.
Mkandarasi aliyekuwepo alituletea nyaraka feki zilizoghushiwa na kulipwa pesa kiasi cha Sh bilioni 27 ikiwa ni malipo ya awali jitihada za kuzirudisha tulizifanya na tunefanikiwa.
Kufanikiwa bado maana hazijarejeshwa.
 
Waziri Aweso, mradi wa maji Magadini - Makiwaru, uliopi wilaya ya Siha, bili za maji wateja wanalioia CRDB Bank badala ya kulipia kwa control number. Upigaji ni mkubwa.
 
1) Alifoji vipi?
2) mfadhili ni nani? Kwamba mtoa fedha sio serikali?
3) mtu anafoji vipi malipo ya 27Bil bila watu wa serikali kujua?
 
Tuna shida gani nchi hii. Inawezekanaje kulipwa mabilioni hayo yote bila uhakiki. Kuna watu wanatakiwa waende ndani. Hongera pia kwa aliyeweza kuona na pesa kurudishwa Serikalini.
 
Aliyekuwa Mkandarasi wa Mradi mkubwa wa Maji wa Mwanga, Same na Korogwe, Badr East Africa Enterprises Ltd, ameridhia kurejesha fedha za mradi huo zaidi ya Sh bilioni 27 alizodaiwa kughushi na kujipatia isivyo halali.

Mradi huo ambao inatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya laki nne, alighushi nyaraka hizo na kulipwa malipo ya awali na serikali kinyume na taratibu.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya maji, Mhandisi Antony Sanga, wakati Akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo baada ya serikali kusitisha mkataba na mkandarasi huyo.

Akizungumza mbele ya viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Waziri wa Maji, Jumaa Awesu, Mhandisi Sanga alisema Mkandarasi huyo alijipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu.

Alisema mkataba wake ulisimamishwa ili kuchukua hatua ya fedha hizo kurejeshwa na kuendelea na mradi kwa kupata mkandarasi mwingine.

“Mkandarasi aliyekuwepo alituletea nyaraka feki zilizoghushiwa na kulipwa pesa kiasi cha Sh bilioni 27 ikiwa ni malipo ya awali jitihada za kuzirudisha tulizifanya na tunefanikiwa.

“Kazi iliyokuwepo baada yakusimamisha mradi na kukabidhi mkandarasi huyo kwenye vyombo vya dola alikiri kughushi nyaraka na kujipatia fedha hizo mpaka sasa yupo ndani na sheria unaendelea kufuatwa,” alisema.

Alisema wafadhili waliokuwa wakifadhili mradi huo waligoma kuendelea kutoa fedha za kuendelea na ujenzi kwa masharti ya fedha za awali zilizolipwa kwa wakandarasi zirejeshwe ili waweze kuendelea jambo ambalo serikali ipo tayari na italipa bilioni mbili.

Akizungumza na viongozi hao,Waziri Aweso, alisema mkandarasi huyo amekubali kurejesha kiasi hicho cha fedha ambapo utekelezaji wa mradi ambapo aliwatakana wataalamu wa maji kuacha tabia ya kuongeza gharama kwenye miradi kwa maslai binafsi.

“Kwa sasa fedha zinarudishwa lakini nawaomba wataalamu muache tabia ya kuongeza gharama kwenye miradi ya maji fedha hizi ni za wananchi hatuwatendei haki lakini pia miradi ya maji sio ya wizara viongozi wote mnahaki ya kuitembelea maana nataka uwazi,” alisema Aweso.

Mtanzania
Hivi Mkandarasi aluvunja benki kwenda kuzichukua?
Kuna watu wskubwa wizarani ni lazima walishiriki hiyo hewa.
 
1) Alifoji vipi?
2) mfadhili ni nani? Kwamba mtoa fedha sio serikali?
3) mtu anafoji vipi malipo ya 27Bil bila watu wa serikali kujua?
Fursa fursana... Mwisho wa siku sote tunahitaji pochi nene... Hivyo penye loop hole unapatumia vilivyo

Mmh amerudisha bila kushtakiwa? Kimyakimya? Amepewa adhabu gani kwa kosa la kughushi?
Adhabu zipo kwa ajili ya masikini na wanyonge wa ccm kama wale vibaka wakwapuaji Manzese na wezi wa kuku. Huyo tajiri hazimhusu
 
Huyu alilipwa wakati wa Shetani Magufuli. Mihela yote hiyo mradi hewaa. Huyu Mliwa funza ndio mwizi mwendazake Magufuli. Hiyo ni trailer tu siku ukisikia madudu ya Stieglers Goji ndo mtaharisha.
 
Back
Top Bottom